loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tusaidieni kukomboa vifaa vyetu -TAHA

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama hicho Nicholaus Mihayo alisema wanadaiwa Sh 1,000,000 ili waweze kutoa vifaa hivyo ambavyo wametumiwa na chama cha dunia cha mchezo huo.

“Naomba wadau watusaidie fedha kwa ajili ya kutoa vifaa bandarini kwani chama chetu kimeshindwa kutokana na ukata unaotukabili”, alisema Mihayo.

Mihayo alilishukuru Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwa kuwapa Sh 500,000 kama sehemu ya mchango wao ili waweze kuchukuwa vifaa hivyo, ila akawaomba wadau wengine hata mtu mmoja mmoja kuwasaidia.

Vifaa vilivyopo bandarini ni mipira 100 ya mchezo huo pamoja na fulana ambazo zitapelekwa kwa vyama vya mikoa ili kuendeleza mchezo huo ambao unaonekana kupoteza umaarufu.

Pia alisema kuwa chama chake kina mpango wa kuandaa michezo itakayoshirikisha mikoa mbalimbali kwa lengo la kupata vipaji vipya vitakavyounda timu ya taifa.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi