loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuwaokoe wasichana ndoa za utotoni kwa vitendo

Msichana huyo alisimulia kwamba baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha IV shule ya sekondari Uroki mwaka jana, baba yake alimweleza kuwa ameshamtafutia mchumba aolewe na kutimiza azma hiyo tarehe iliyotajwa.

Lakini kwa maelezo yake msichana huyo alikuwa hayuko tayari kwa mahusiano ya ndoa, kwa kuwa bado anataka kujiendeleza kielimu licha ya ukweli kwamba umri wake bado mdogo kisheria kuingia katika jambo hilo.

Baada ya kupata taarifa hizo kwa njia ya simu, DC alimuagiza ofisa elimu kuongozana na polisi kwenda kumchukua mtoto huyo mahali alikoolewa. Hivi sasa anaishi nyumbani kwa DC huyo.

Taarifa zinasema kuwa huyo ni mtoto wa tatu kuokolewa na DC kutoka ndoa za utotoni.

Ni wazi kwamba bado tupo katika safari ndefu ya kukabiliana na mila na desturi potofu dhidi ya watoto wa kike ambao kama walivyo wenzao wa kiume wanastahiki kusoma hadi kufikia uwezo waliojaliwa na Mungu katika ngazi za elimu.

Nani hajui elimu ni ufunguo wa maisha au usemi maarufu usema 'Ukimuelimisha mwanamke unaelimisha taifa zima?'

Kwa nini matukio ya aina hii hurudiwa mara kwa mara kwa watoto wetu wa kike? Kuna mikakati gani ya kitaifa kuweza kukabiliana na jambo hili?

Kama Mzazi naamini kabisa kwamba iwapo kutakuwa na ushirikiano na mshikamano wa kutosha kati ya jamii, wazazi, walezi, viongozi wa serikali, dini na siasa inawezekana kulidhibiti jambo hili.

Mfano ni kama huu wa DC wa Kiteto. Amewezesha kunusuru wasichana watatu.

Je, kama wakuu wa wilaya wote na viongozi wengine katika ngazi hiyo wangechukua hatua kama alivyofanya mwenzao wa Kiteto, huenda tatizo hili lingedhibitiwa vilivyo.

Hatujachelewa, tujipange vizuri kuanzia ngazi za vijiji, kata, wilaya na hadi mkoa na taifa kulipiga vita suala hili kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote.

Nani kawaambia watoto wa kike kazi yao ni kuolewa tu na siyo vinginevyo? Mitazamo hasi kama hiyo haina budi kupigwa vita kwa sababu haina mashiko yoyote kwa msichana husika, familia yake na hata kwa taifa.

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Nicodemus Ikonko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi