loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Twiga Stars kuivaa Zambia Feb 15

Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma kuanzia saa 9 kamili kwa saa za Zambia na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda.

Wambura alisema Mukansanga atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake; Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na Angelique Tuyishime.

Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka Namibia.

‘Twiga Stars iliingia kambini jana kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Zambia ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za AWC zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Awali, timu hiyo ilikuwa iingie kambini Januari 15, mwaka huu, lakini hali ilikuwa tofauti na hakuna sababu zilizotolewa kwa nini kambini iliahirishwa.

Hata hivyo, kutokana na umuhimu wa mchezo huo, Kocha Mkuu Rogasian Kaijage alishaanza mazoezi tangu wiki iliyopita wakitokea nyumbani na kurudi kwa wale wenyeji wa Dar es Salaam.

Kaijage amewaita kikosini wachezaji 30, ambao ni Amina Ally, Amisa Athuman, Anastazia Anthony, Asha Rashid, Aziza Mwadini, Belina Julius, Donisia Daniel, Esther Chabruma, Evelyn Sekikubo, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Issa na Fatuma Mustapha.

Wengine ni Fatuma Omari, Happiness Hezron, Maimuna Hamisi, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Najiat Abbas, Neema Paul, Pulkeria Charaji, Semeni Abeid, Shelder Boniface, Sophia Mwasikili, Theresa Yona, Vumilia Maarifa na Zena Khamis.

KLABU ya Simba  imetambulisha  mashindano mapya ya Super  Cup, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi