loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Twiga Stars yaahidi makubwa Zambia

Twiga Stars inakabiliwa na mechi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Zambia ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Akizungumza wakati wa kuwaaga wachezaji wa Twiga, Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi alisema ana imani na timu hiyo kwani ina wachezaji ambao wamekaa pamoja kwa muda mrefu.

“Nakumbuka 2011 timu hii ikiwa na baadhi ya wachezaji ambao nawaona hapa ilishiriki kwenye mashindano ya Olimpiki Afrika hivyo naamini itafanya vizuri”, alisema Bayi.

Pia Bayi alimpongeza Kocha Kaijage kwa kazi yake nzuri ya kufundisha na kurejesha heshima kwa timu hiyo ambayo inaonekana kuwa ni imara huku wachezaji wake wakiwa nadhifu.

Naye kocha Kaijage alisema anashukuru timu yake ipo vizuri kwani imejiandaa vya kutosha hivyo wana uhakika watakwenda kufanya vizuri.

Nahodha wa timu hiyo, Sophia Mwasikili alisema wanaamini watafanya vizuri kulingana na mazoezi waliyoyapata kutoka kwa kocha wao ila dua na sapoti za watanzania zinahitajika ili wafanye vizuri zaidi.

“Sisi tupo vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo huo wa ugenini ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kusonga mbele ila tunawaomba watanzania watupe sapoti na dua zao”, alisema Sophia.

RUVU Shooting, Kagera Sugar na Gwambina ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi