loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchenjuaji dhahabu waingiza mil.861/-

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umewezesha Serikali kukusanya kiasi hicho, kutokana na ukaguzi huo unaofanyika Jijini Mwanza na katika Mji wa Geita.

Kiasi hicho ambacho ni wastani wa makusanyo ya Sh milioni 123 kwa mwezi, kimetokana na ubunifu na ushirikiano unaofanywa baina ya Wakala, Ofisi za Madini na wananchi waliowezesha upatikanaji wa taarifa juu ya kuwepo kwa mitambo ya kuchenjua dhahabu katika maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa kutoka TMAA imefafanua kwamba walibuni utaratibu wa kutumia lakiri, ambazo zinawekwa kwenye mitambo ya kuchenjulia dhahabu inayojulikana kama elution plants.

Kutokana na TMAA kutumia utaratibu huo wa lakiri, mmiliki wa mtambo wa kuchenjua dhahabu, analazimika kuwasiliana na wakaguzi wa mamlaka na Ofisi ya Madini husika ili kuweza kufanya uchenjuaji.

KAMPUNI ya uchimbaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi