loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchu wa mapenzi husababisha duma jike kuishi peke yake

Hukimbia kilometa 113 kwa saa. Mbio hizo ndizo zinazomuwezesha kupata chakula ikilinganishwa na wanyama wengine wala nyama ambao huweza kunusa palipo na windo kisha kulinyemelea.

Duma wanapatikana zaidi ukanda wa bara ya Afrika na baadhi ya sehemu katika bara la Asia na chakula chake kikuu ni wanyama jamii ya swala ingawa anaweza kula wanyama wengine pia.

Duma ana urefu sentimita 125 hadi 165 na mkia wake unakaribia urefu wa setimita 60 hadi 110. Urefu wa mabega ni sentimita 45 hadi 80.

Duma dume ni wakubwa kwa asilimia 30 zaidi ukilinganisha na jike. Uzito wa duma dume ni kati ya kilogramu 37 hadi 91 wakati duma jike ana uzito kati ya kilogramu 28 hadi 60.

Duma wenye miili mikubwa hupatikana kwenye maeneo yaliyojitenga na wanyama wengine wala nyama hasa toka kwa wale jamii ya paka wakubwa waliozoeleka kama vile simba na duma wakubwa wenye milia, yaani tiger.

Ingawa baadhi ya watu huwachanganya duma na paka wengine wakubwa wenye madoa hasa chui na jaguar, ipo tofauti kati ya wanyama hao na unaweza kuwatambua kwa kuangalia mitindo tofauti ya madoa yao.

Wataalamu wa masuala ya wanyama wanabainisha kuwa duma wana madoa ya kawaida yaliyosambaa mwili wote, jaguar ana madoa madogo ndani ya vijimiraba; wakati chui ana madoa ndani ya miduara midogo kuliko ile ya jaguar. Duma ngozi yake ni rangi ya njano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi.

Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake paka wakubwa kama chui. Ana macho makubwa yaliyozungukwa na mstari mweusi maarufu kama mstari wa machozi ambao unazu nguka pia pua na mdomo.

Mstari huo humuwezesha kuzuia miale ya mwanga wa jua usiingie machoni pia humsaidia kuona umbali mrefu. Mwili wake mwepesi unamsaidia kukimbia kwa mwendo kasi na kukamata lindo hata kama liko umbali mrefu.

Ana uwezo wa kuwinda akiwa katika msitu mnene tofauti na wanyama wengine ambao huwinda wanyama katika eneo lisilokuwa na msongamano mkubwa wa miti na vichaka. Duma mkubwa ana uzito wa kilo kati ya 21 hadi 72.

Mwili wake una urefu wa sentimita 110 hadi 150 sawa na nchi 34 hadi 59 na mkia wake una urefu wa sentimita 60 hadi 84 sawa na nchi 24 hadi 33. Mabega ya dume yana urefu wa setimita 66 had 94 ina inaelezwa kuwa mabega ya dume ni makubwa zaidi ikilinganishwa na ya jike ila mikia yao ina urefu sawa.

Wataalamu wanasema vipimo pekee ndio vinavyobainisha tofauti ya ukubwa wa duma jike na dume kwa sababu ukiwaangalia katika hali ya kawaida unaweza kudhani kimo chao ni sawa.

Kwa mujibu wa historia ya mnyama huyo alipatikana katika bara la Afrika kati ya miaka milioni 26 hadi 7.5 milioni iliyopita.

Kuna aina sita za duma wanaopatikana sehemu mbalimbali duniani ila wanatofautiana kidogo kulingana na mazingira wanayoishi. Duma jike na duma dume hupevuka akiwa na umri wa mwaka mmoja na mienzi nane. Hata hivyo, duma dume akishapevuka hawezi kupanda jike hadi atakapofikia umri wa miaka mitatu.

Inaelezwa kuwa duma hawana msimu maalum wa kuzaliana hivyo hujamiiana wakati wowote pale jike linapopata joto. Ripoti ya mwaka 2007 kuhusu utafiti uliofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inasema kuwa duma jike hawana uaminifu katika masuala la mapenzi kwani hupenda kujamiiana na madume tofauti.

Madume hutumia mkojo hujiwekea mipaka katika himaya kwa lengo la kuzuia mwingiliano katika mahusiano na majike. Hata hivyo, utafiti huo unaonesha kuwa majike huingia kwenye himaya za madume tofauti na baada ya kujamiiana huondoka. Kwa kuwa majike yanapenda kupandwa na madume tofauti hivyo duma mmoja anaweza kuwa na watoto wenye baba tofauti.

Inadaiwa kuwa uchu wa mapenzi ni moja ya sababu ya duma jike kupenda kuishi peke yake kwa maana ya kutotaka kudhibitiwa na dume.

Baada ya kujamiiana dume jike hubeba mimba kwa siku 90 hadi 98 sawa na miezi mitatu hadi miezi mitatu na wiki moja. Huzaa watoto kati ya watatu hadi wanane.

Endapo watazaliwa watoto wanane watatu au wanne hufa wangali wadogo. Inaelezwa kuwa watoto wanaobahatika kukua na kuishi ni wanne au watano ambao huzaliwa wakiwa na uzito wa gramu 150 hadi 300.

Tofauti na wanyama wengine wa kundi la paka wakubwa, watoto wa duma huzaliwa wakiwa na madoa katika ngozi zao. Pia huwa na manyoya malaini sehemu ya shingoni.

Utatifi wa kisayansi unaonesha kuwa manyoya hayo huwafanya watoto wa duma kuonekana kama kitu kisicho cha kawaida hivyo huwasaidia kujikinga dhidi ya maadui wakati wa utoto. Manyoya hayo hutoweka kadiri mtoto wa duma anavyokua.

Watoto wa duma hukaa chini ya uangalizi wa mama zao hadi wanapofikia umri wa miezi 13 hadi 20. Mama yao huondoka na kuwaacha watoto peke yao na huendelea kukaa katika kundi kwa miezi sita bila mama yao.

Baada ya hapo watoto wa kike kuondoka na kila mmoja kushika njia yake ili kutafuta chakula na madume. Duma wana mfumo wa ajabu katika mahusiano. Duma jike wakishapevuka hutawanyika kila mmoja hushika njia yake kutafuta madume. Duma dume huendelea kukaa pamoja katika kipindi cha maisha yao yote.

Ikiwa katika uzao kulikuwa na dume moja basi italazimika kujiunga na dume mwingine ambaye alizaliwa peke yake au kujiunga na kundi la madume wa rika lake. Inadaiwa kuwa wivu wa mapenzi husababisha duma jike kuishi maisha ya upweke kwa kuwa wakiwa katika hali ya kawaida hawachanganyiki.

Jike kijana anaweza kuanzisha urafiki na mama yake ila urafiki huo hudumu kwa muda mfupi hasa wanapokuwa kwenye kipindi cha joto ambapo kila mmoja hushika njia kutafuta dume na hawarudi tena kukaa pamoja.

Majike wenye watoto huunda ujamaa kwa kukaa pamoja kipindi cha kulea watoto. Hata hivyo inaelezwa kuwa huenda ujamaa huo ni mahususi kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maadui kwa kuwa kila mmoja huwinda peke yake na kulea watoto wake pasipo kushirikiana.

Watoto wakishakua ujamaa wa kuishi pamoja unakwisha na kila mmoja kushika njia zake kuendelea na maisha ya upweke huku wakitafuta madume kwa ajili ya kujiandaa na kipindi kingine cha uzazi. Ingawa madume huishi katika makundi hawachanganyiki na majike hata mara moja ila wakati wa kujamiiana.

Jike akipata joto hutoa harufu inayomvutia dume na hapo hukutana eneo maalum na baada ya kujamiiana kila mmoja hushika njia yake na huenda wasikutane tena kwa kipindi cha maisha yao yote kwa kuwa majike hupendelea kupandwa na madume tofauti.

Malezi ni jambo muhimu kwa watoto wa duma. Katika kipindi cha kwanza cha miezi minane watoto wa duma hutakiwa kujifunza mambo mengi kutoka kwa mama zao na mafunzo hayo ndio msingu mkuu katika maisha. Watoto wa duma wakishafika umri wa majuma matano hadi sita hufuatana na mama zao kwenye mawindo ili kujifunza mbinu za kuwinda.

Maisha ya duma yanategemea sana mafunzo na uhodari wa kujifunza mbinu za uwindaji na jinsi ya kujihami dhidi ya maadui.

Wastani wa maisha ya duma ni miaka 12 ila duma wanaofugwa kwenye hifadhi ya wanyama huweza kushi hadi miaka 20. Kwa kawaida Duma hana maadui wengi ila watoto wake huweza kuwindwa na simba, fisi na wanyama wengine wanaokula nyama hasa wa Afrika na wale wa Asia.

Lengo ni kuwapunguza katika kugombea chakula. Ingawa duma hawana maadui wengi kama wanyama wanakula majani, ripoti ya Muungano wa Uhifadhi Duniani (IUCN) inasema wanyama hao wapo katika orodha ya wanyama walioko katika hatari ya kutoweka kutokana na uharibifu mbalimbali wa mazingira, uwindaji haramu na idadi kubwa ya vifo vya watoto wa duma.

Ni wajibu wetu sote kutunza mazingira na kulinda hifadhi za taifa ili kuwezesha duma kuendelea kuwa miongoni mwa urithi wa Tanzania. Makala haya yameandaliwa na Kaanaeli Kaale kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya habari kwa msaada wa mtandao wa kompyuta.

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya ...

foto
Mwandishi: Kaanaeli Kaale

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi