loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uchumi wa Tanzania wakua kwa asilimia 7

Mauro katika taarifa yake kwa vyombio vya ha bari jana, alisema Tanzania ina matarajio mazuri ambapo uchumi unatarajia kuendelea kukua kwa kasi hiyo hiyo kwa mwaka mzima.

“Mfumuko wa bei ulipungua hadi asilimia 6.1 Septemba ambapo ukiondoa bei za vyakula na mafuta ulipungua hadi asilimia 5.8,” aliongeza.

Kutokana na mwelekeo mzuri wa bei za ndani za vyakula na mwendelezo wa sera, fedha inayolenga utulivu wa bei, matarajio ni mfumuko wa bei kuendelea kushuka hadi asilimia 5 katikati ya mwaka ujao ambalo ni lengo la muda wa kati la nchi, ilisema taarifa.

Ilisema nakisi ya urari wa mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi imepungua kiasi hadi asilimia 13½ ya Pato la Taifa kwa kipindi cha Julai 2012 na Juni mwaka huu, ingawa kiwango hicho bado ni kikubwa.

Hata hivyo, Mauro alisema kulijitokeza hali ya matumizi makubwa ya Serikali isivyotarajiwa katika mwaka wa fedha uliopita ( 2012/13, Julai hadi Juni, matokeo yake, kiwango halisi cha ukopaji wa serikali kutoka taasisi za ndani kilizidi lengo lililokubaliwa chini ya mpango wa Serikali na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa asilimia moja ya Pato la Taifa.

“Kwa mwaka huu wa fedha (Julai 2013 hadi Juni 2014), makusanyo ya kodi yanaweza kuwa chini ya makadirio ya mwanzoni. Hili linaweza kusababisha kuhitajika kwa marekebisho makubwa katika bajeti wakati wa kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha nusu mwaka ili kuufanya mpango wa matumizi uendane na upatikanaji wa mapato,” iliusema taarifa.

Kuhusu Serikali ilisema ilisisitiza ahadi yake ya kutovuka lengo la nakisi ya bajeti ya asilimia tano ya Pato la Taifa ambapo ili kuendelea kukuza uchumi na kuzuia matumizi makubwa isivyotarajiwa kwa mwaka huu wa fedha na mwaka ujao, vipaumbele vitakuwa kuongeza mapato kwa kupunguza na kurahisisha misamaha ya kodi na kutatua matatizo ya kifedha yanayoikumba sekta ya nishati.

Ilisema changamoto za kisera katika muda wa kati ni kuendelea kukuza uchumi kwa kuwekeza katika miundombinu ya uzalishaji, kulinda matumizi kwenye vipaumbele vya huduma za jamii, kuhakikisha deni la Taifa linaendelea kuwa himilivu.

Nyingine ni kuimarisha mfumo wa kitaasisi ili kuhakikisha mapato yatakayotokana na gesi iliyogunduliwa yananufaisha wananchi wote, na kuboresha mazingira ya biashara.

“Majadiliano yataendelea katika wiki zijazo; mkutano ujao wa Bodi Tendaji ya IMF kuhusu Tanzania umepangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao. Ujumbe wa IMF unatoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa ukarimu wake na kwa majadiliano ya uwazi na yenye tija kwenye masuala ya kisera.”

Ujumbe huo ulikuwa nchini kuanzia Oktoba 23 kwa madhumuni ya kufanya majadiliano na Serikali chini ya kanuni ya nne ya mkataba ulioanzisha IMF.

Ulikuwa ukifanya tathmini ya mpango wa ushauri chini ya Mkopo Nafuu wa Dharura na kuanza majadiliano juu ya uwezekano wa kuwa na mpango mpya wa Ushauri wa Sera za Uchumi (PSI).

Ulikutana na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Benno Ndulu, na maofisa waandamizi wa Serikali.

Majadiliano yalijumuisha mapendekezo yaliyopatikana wakati wa vikao vya kuchangia mawazo juu ya vipaumbele katika sera za kiuchumi za muda wa kati vilivyofanyika Agosti kati ya IMF, Serikali, BoT, wabunge, sekta binafsi, asasi za kiraia, na washirika wa maendeleo.

TANZANIA na Burundi zimetiliana saini makubaliano katika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi