loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Udhibiti mkali filamu za matusi, maigizo

Yeyote atakayetenda kosa hilo atashughulikiwa kikamilifu na Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza inayowasilishwa leo bungeni kufanyiwa marekebisho.

Chini ya marekebisho hayo, mtu atakayepatikana na kosa, atakabiliwa na adhabu ya kulipa faini ya Sh milioni tatu kutoka ile ya awali ya Sh 15,000 au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela badala ya mwaka mmoja wa awali.

Sheria hizo ziko kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 3 wa Mwaka 2013, ambao unawasilishwa bungeni leo, ukijumuisha sheria mbalimbali 15, kwa lengo la kuondoa upungufu uliobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo.

Muswada huo utakaowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, katika Sehemu ya Tano unahusu sheria hiyo ya Filamu na Michezo ya Kuigiza.

Katika marekebisho hayo, sheria hiyo imeonekana baadhi ya vipengele vyake vimepitwa na wakati kwa kuwa adhabu ni ndogo kuliko ukubwa wa kosa na hivyo masharti mapya yamewekwa kwa ajili ya kuwa na sheria madhubuti.

Muswada wa sheria hiyo ambao nakala yake gazeti hili inayo, adhabu imeongezeka kutoka Sh 15,000 hadi kufikia Sh milioni tatu.

Kadhalika kwa upande mwingine, adhabu ya kifungo nayo imeongezeka kutoka mwaka mmoja hadi kufikia miaka miwili, kwa watu watakaopatikana na kosa la kutoa lugha au kauli za uchochezi kupitia filamu na michezo ya kuigiza na kwamba adhabu hizo zinaweza kutekelezwa kwa pamoja.

Ongezeko la adhabu hiyo ni baada ya Kifungu cha 34(1) cha sheria hiyo kufanyiwa marekebisho. Kwa mujibu wa marekebisho hayo, hatua hiyo itapunguza au kuondoa lugha na kauli chafu na za uchochezi zinazotolewa na watu au vikundi vya watu kupitia filamu na michezo ya kuigiza.

Hata hivyo, vifungu vingine vya sheria hiyo havijafanyiwa marekebisho kutokana na kuonekana kuwa havijaleta mkanganyiko wakati wa utekelezaji.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi