loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ufuatiliaji magari kielektroniki uanze mapema

Lengo la utaratibu huo ni kuhakikisha bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi, hazifunguliwi njiani na kuingizwa katika soko la ndani, kwa lengo la kukwepa kodi, Taarifa hiyo ilitolewa mjini Dodoma na Mchumi Mwandamizi wa Idara ya Maendeleo Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Vedastus Manumbu.

Tunaunga mkono tamko hilo kwa sababu utaratibu huo utaondoa kero nyingi zilizopo hivi sasa kwa wasafirishaji wanaposafirisha bidhaa mbalimbali. Tungependa utekelezaji wa utaratibu huo, uanze haraka iwezekanavyo.

Pia, tungependa elimu ianze kutolewa kwa wadau mbalimbali, watakaohusika katika kutekeleza utaratibu huo, kama vile Serikali yenyewe, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mawakala wa forodha.

Tunashauri hatua hiyo iende sambamba na ujenzi wa vituo vingi vya kisasa vya ukaguzi wa magari na mizigo nchini. Ni vema Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, ushirikiane na Kitengo cha Biashara cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuhakikisha kuwa vituo hivyo vya ukaguzi wa magari, vinajengwa haraka.

Vituo vya kisasa tulivyotangaziwa muda mrefu kuwa vitajengwa, basi vijengwe haraka ili kukagua magari ya mizigo na abiria. Vituo hivyo ni pamoja na vya Vigwaza, Manyoni na Nyakanazi.

Tuna uhakika vituo hivyo vya kisasa vya ukaguzi wa magari ya mizigo na abiria, vikijengwa haraka, basi vitapunguza vizuizi vya barabarani nchini, ambavyo mwaka 2008 vilikuwa 55 na sasa vimebaki vizuizi 15.

Kwa sasa moja ya mambo ambayo yanalalamikiwa mno na wasafirishaji nchini ni foleni ndefu kwenye vituo vya ukaguzi wa magari ya mizigo na abiria, kwa mfano Kituo cha Kibaha.

Wasafirishaji wanasema Kituo hicho cha Kibaha, kimekuwa kero kwao na kinazorotesha biashara. Wanasema wanapoteza muda mrefu kukaguliwa katika kituo hicho, hali ambayo itarekebishwa kwa kujenga kituo cha kisasa.

Wasafirishaji nchini pia wamekuwa wakilalamikia mizani iliyopo katika vituo vingi. Wanasema matumizi ya mashine za kielektroniki yataondoa tatizo hilo.

Aidha, wasafirishaji wengine wanahoji kwa nini ujenzi wa Kituo cha Vigwaza, umechukua muda mrefu. Wanasema ni vema mkandarasi anayejenga Kituo cha Vigwaza, ahimizwe kukamilisha mapema ujenzi huo ili kuondoa kero wanayoipata katika Kituo cha Kibaha.

Tunatarajia pia ujenzi wa vituo vingine viwili katika maeneo ya Manyoni Mkoa wa Singida na Nyakanazi mkoani Kagera, utaanza haraka ili kupunguza gharama na muda wa usafirishaji wa mizigo na abiria na pia kulinda ubora wa barabara nchini. Kwa hakika, ufuatiliaji wa magari kielektroniki, utaleta manufaa mengi.

Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi