loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uholanzi yapeta, Nigeria, Algeria kazi leo

Iitokana na kuangushwa kwa Arjen Robben na mlinzi na nahodha wa Mexico, Rafael Marques.

Huntelaar aliingia badala ya Robin van Persie Uholanzi ilisawazisha katika dakika ya 87 kwa bao safi la shuti kali lililofungwa na Wesley Sneijder, kusawazisha bao la mapema na mshambuliaji Giovani do Santos katika dakika ya 49.

Katika hatua nyingine, timu mbili za Afrika zilizobaki katika fainali za Kombe la Dunia la Fifa zinashuka dimbani leo zikiwania tiketi ya kucheza robo fainali. Mabingwa wa Afrika, Nigeria wataikabili Ufaransa kuanzia saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki wakati Algeria itakumbana na Ujerumani saa tano usiku.

Ufaransa itakabiliana na mtihani mkali tangu kuanza kwa fainali hizo kwa kuikabili Nigeria baada ya kuwa kikosi hicho cha Didier Deschamps kimefuzu kirahisi katika Kundi E.

Ushindi dhidi ya Honduras na Uswisi uliwawezesha kusonga mbele, huku Deschamps akiwapumzisha nyota wake kadhaa katika mechi ya mwisho dhidi ya Ecuador ambayo walitoka nayo sare ya 0-0.

Wakati Nigeria ilianza kwa kusuasua, lakini ikafuzu utoka katika kundi lililokuwa na timu za Argentina, Bosnia- Herzegovina na Iran.

Hiyo ndio maana kiungo Yohan Cabaye – ambaye anatarajiwa kurejea dimbani baada katika mechi ya leo Brasilia baada ya kutumikia adhabu ya kadi mbili, anasema Ufaransa inaingia dimbani ikiwaheshimu wapinzani wao.

“Hatua moja mbaya, unajikutana nyumbani, kwa hiyo unakuwa na presha hiyo,” alisema.

“Naiheshimu timu hii ya Nigeria na tunaweza kusonga mbele, lakini kusema unaweza kushinda Kombe la Dunia…lazima uwe mwangalifu.”

Kwa Nigeria, kazi ya Stephen Kesi inaendelea kuleta matunda. Mlinzi huyo wa zamani ameiongoza Super Eagles kutwaa taji la Mataifa ya Afrika na kufika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, ikiwa haijafanya hivyo tangu mwaka 1998.

Victor Moses na Godfrey Oboabona wanaweza kucheza leo baada ya kuwa fiti na kukaa benchi dhidi ya Argentina, ingawa Michel Babatunde hatakuwamo.

Kwa Ufaransa, Mamadou Sakho hayuko fiti sana. Kwa Ujerumani, Kocha Joachim Low anafahamu kuwa hawapaswi kuzembea kama wanataka kuepuka kudhalilishwa na Algeria.

Wakati Ujerumani imewahi kutwaa ubingwa mara tatu, Algeria inacheza hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia yao, na ushindi kwa timu hiyo ya kaskazini mwa Afrika, matokeo yake yatakuwa moja ya matokeo ya kushangaza katika historia ya Kombe la Dunia.

Ujerumani – moja ya mataifa makubwa katika soka duniani – bila ya shaka itaanza mechi hiyo ya raundi ya pili mjini Porto Alegre ikipewa nafasi kubwa ya kuingia robo fainali. Hata hivyo, kocha Low anaamini itakuwa dharau kubwa kwa timu yake kuichukulia mechi hiyo kirahisi.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: FORTALEZA, Brazil

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi