loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ujenzi wa mkongo kugharimu mamilioni

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba aliliambia Bunge jana kuwa fedha hizo za mkopo wa masharti nafuu, zilitolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.

Aidha, alisema mkongo huo ulianza kutumika Juni 2010 mara baada ya kukamilika awamu ya kwanza ambayo ilijumuisha mikoa ya Dares Salaam, Morogoro, Pwani, Iringa, Dodoma, Singida, Manyara, Kilimanjaro,Tanga, Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara na Kagera.

Alisema awamu ya pili ilikamilika na kuanza kutumika Juni 2012 na ilihusisha mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa,Ruvuma, Mtwara na Lindi.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kusini, Desderius Mipata (CCM), ambaye alitaka kujua ujenzi wa Mkongo wa Taifa umeigharimu serikali kiasi gani cha fedha za kigeni. Pia, alihoji kwa nini mpaka sasa mkongo huo haujaanza kutumika.

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi