loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukatili wa kijinsia bado kero Manyara

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Mwajabu Nyamkomolo alisema hayo jana mjini Babati wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia na watoto.

Alisema mkoa wa Manyara umekuwa nyuma kimaendeleo hasa kwa wanawake kwa sababu ya ukatili na unyanyasaji wanaofanyiwa. Alisema sababu kubwa zinazochochea ukatili huo ni mila na desturi, zinazomkandamiza mwanamke zinazowafanya wanawake wengi kutokuwa na maamuzi.

Alisema kuna imani iliyojengeka kuwa mwanamume pekee ndiye wenye maamuzi ya mwisho katika familia. Alisema watu wengi bado hawaielewi dhana ya jinsia na hivyo kusababisha watu kudhani mwanamke hawezi kufanya chochote. Pia watoto wa kike hunyimwa haki ya kusoma na kulazimishwa kuolewa.

Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoani humo, Anna Fissoo alisema wataendelea kutoa elimu shuleni kwa watoto wa kike kwa kushirikiana na taasisi binafsi ili wajue kuwa vitendo wanavyofanyiwa ni vya kikatili na wawe wanatoa taarifa pindi wanapotaka kufanyiwa ukatili.

Mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji. Takwimu zinaonesha asilimia 70 ya watoto wa kike wa kuanzia miaka mitano hadi 15 wamekeketwa.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi