loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukawa: Hatutasusia Katiba

Alisema hayo mjini hapa jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa kikao cha Umoja huo kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.

Alisema wataendelea kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba bora na yenye kuzingatia maslahi ya Watanzania na si kikundi cha watu wachache.

Alisema itakuwa ni jambo la ajabu kwao, kususia mchakato wa uundaji wa Katiba mpya wakati vyama vya upinzani na asasi za kiraia, ndiyo chimbuko la madai ya kutaka kuwepo kwa mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya.

“Ni dhamira ya kundi hili kuona mchakato wa Katiba unafanikiwa na kuifanya Tanzania inakua na Katiba bora. Tumefanya uvumilivu mkubwa lakini kama inavyofahamika uvumilivu una mwisho.

“Tunataka kuendelea kushiriki katika mchakato huu hadi pale Watanzania watakapoona nia ovu ya kuona Katiba mpya na bora haipatikani niya akina nani. Si lengo letu kupoteza fedha za Watanzania, tutaendelea kushiriki hadi pale uvumilivu utakapotushinda.

“Tukijiridhisha kwamba tumeshindwa tutawaambia Watanzania ni nini cha kufanya na tuna imani nia yetu ya kuwa na Katiba bora itaonekana wakati tutakapoingia kwenye vifungu vya rasimu,” alisema Mbowe.

Akizungumzia hatma ya mchakato huo, Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Profesa Ibrahim Lipumba alisema ;

“ Sisi tumekuja hapa Dodoma kuandika Katiba ya wananchi. Hatuwezi kuondoka ili kuwaachia watu waandike Katiba ya CCM”.

Kauli hizo za viongozi wa Ukawa, zimekuja wakati kukiwa na wasiwasi kwamba wanataka kususia mchakato huo wa uandaaji wa Katiba mpya, kwa madai ya kuhofia kumezwa na wabunge wa CCM. Hata hivyo hoja hiyo imekuwa ikiondolewa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta ambaye ametaka wabunge kutanguliza nia njema katika mchakato huo.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Joseph Lugendo na Oscar Mbuza, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi