loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukawa wajipanga uchaguzi Serikali za Mitaa

Katika taarifa ya pamoja ya Ukawa, vyama hivyo: Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, vimejihimiza kuhakikisha vinanyakua nafasi kwenye uchaguzi huo kwa lengo la kujiandaa na uchaguzi mkuu.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na wenyeviti wa vyama husika, inataka wanachama na viongozi kufanya maandalizi kwa pamoja kwa ajili ya Uchaguzi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliotangazwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu.

“Uchaguzi huo uwe ni fursa ya kwanza ya kuiondoa CCM katika utawala wa nchi yetu kabla ya kuiondoa kabisa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015,” ilisema sehemu ya taarifa iliyosainiwa na Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR Mageuzi) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF).

Wakati huo huo, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amedai uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusema haina mamlaka kuamua kiwango cha mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba kufanya maboresho au marekebisho katika rasimu ya katiba mpya ni kukwepa lawama za Ukawa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Uamuzi wa jana wa Mahakama ulibaki katikati ukakwepa lawama za Ukawa na CCM, kwa maana pamoja na uamuzi wao bado hawakufafanua mipaka ya bunge ni ipi", alisema Lissu.

Akijibu Chadema inahusika vipi na kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea, Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe alisema suala sio Kubenea bali ni aina ya kesi iliyofunguliwa kama ina maslahi ya taifa.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi