loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukuaji Pato la Taifa waongezeka

Taarifa hizo za ukuaji wa Pato la Taifa, zilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Morrice Oyuke wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Hata hivyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi Dk Stephen Kirama alisema yako malalamiko kuwa uchumi unakua lakini haumnufaishi mtu mmoja mmoja.

“Ni jambo ambalo pia linaweza kuangaliwa na kutiliwa mkazo, kuna umuhimu wa kusimamia sera kukuza uchumi kupitia sekta nyingine pia,” alisema Dk Kirama.

Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotolewa jana, ilionesha katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu, uzalishaji umeme na usambazaji maji umekua kwa kasi ya asilimia 12.6 ikilinganishwa na asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Shughuli za uchukuzi na mawasiliano zilifikia kasi ya asilimia 16.5. Sekta nyingine na asilimia za ukuaji katika mabano ni uchumi na kilimo (1.6), uvuvi (2.5), uchimbaji madini, mawe na kokoto (8.7) na uzalishaji wa bidhaa viwandani (8.5).

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi