loader
Picha

Ulanga yakacha kuendesha ligi miaka miwili

Mbali na Ulanga, Wilaya ya Mvomero licha ya kuchezesha ligi hiyo, timu zilizopata nafasi zimeshindwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya ligi kuanza Agosti 9, mwaka huu kutokana na sababu zisizofahamika.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka, alisema hayo juzi mjini hapa na kuzitaja wilaya zilizotoa wawakilishi wawili ni Kilosa, Kilombero, Manispaa ya Morogoro na Wilaya ya Morogoro.

Semka alisema kamati husika itakutana kujadili jambo hilo kwa kuangalia kanuni zilizopo ili hatua zaidi zichukuliwe kwa Ulanga na Mvomero kwa kushindwa kuwa na timu katika hatua hiyo muhimu.

“Mkoa hauna taarifa za kina kwa wilaya hizo sababu za kupeleka zishindwe kuwa na timu ya mshindi wa kwanza na wa pili katika ngazi ya ligi ya Mkoa,” alisema Semka na kuongeza: “Kwa Wilaya ya Ulanga wao sasa ni mwaka wa pili hawajachezesha ligi za ndani na sababu za kushindwa kufanya hivyo hazijulikani. Mvomero wamechezesha ligi na timu zikapatikana, lakini zimeshindwa kuthibitisha hadi siku ya mwisho,” alibainisha Semka.

Alisema timu zinazoshiriki ligi hiyo zimepangwa kwenye makundi mawili ya timu nne, mbili kutoka Morogoro na nyingine kutoka Halmashauri ya Manispaa na zitatumia uwanja wa Sabasaba mjini hapa.

MABINGWA wa kihistoria Yanga leo wanashuka dimbani kuikabili Tanzania Prisons ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi