loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Umaskini utapungua kilimo, viwanda vikiimarishwa

Katika maeneo hayo, 120 ni Dar es Salaam, 120 ni maeneo ya miji mbalimbali na maeneo 160 ni ya vijijini ambapo jumla ya Kaya 10,186 zilikamilisha mahojiano.

Akizungumzia matokeo hayo kwenye mkutano wa kujadili sera za kuondoa umaskini mapema wiki iliyopita, Meneja wa Takwimu za Mazingira na Uchambuzi wa NBS, Sango Simba anasema lengo la kufanya utafiti huo ni kupata taarifa za mapato na matumizi ya kaya husika, ili ziweze kutumika katika kuandaa na kutathmini sera mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Aidha lengo lake ni kutambua na kuona maeneo gani yanahitaji kupewa vipaumbele ili kuyainua na pia kutambua makundi ya watu yaliyoko kwenye mazingira hatarishi.

Kwa mujibu wa Sango, utafiti huo unaonesha maeneo ya vijijini umaskini bado ni wa kiwango kikubwa, ambapo asilimia 84.1 ya watanzania waishio vijijini ni masikini, ukilinganisha na asilimia 14.4 ya wananchi waishio mijini huku jiji la Dar es Salaam kiwango cha umaskini ni asilimia 1.5.

Katika utafiti huo, kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kwa maeneo ya vijijini ni asilimia 33.3 huku ule wa chakula uliokithiri ukiwa ni asilimia 11.3, jambo ambalo ni tofauti na maeneo ya mijini ambapo kiwango ni asilimia 21.7 kwa umasikini wa mahitaji ya msingi na ule wa chakula ni asilimia 8.7.

Kadhalika, kiwango cha umasikini kinaongezeka kadri idadi ya watoto inavyoongezeka katika kaya ambapo kaya isiyo na watoto kiwango cha umaskini ni asilimia 19.8, ukilinganisha na kaya yenye watoto watatu au zaidi ambapo kiwango cha umaskini ni asilimia 40.8

Akizungumzia umaskini wa kipato, Sango anasema matokeo hayo yameonesha kuwa kuna tofauti kubwa ya kipato kwa watu wa mijini na vijijini na kwamba matumizi ya watu wenye uwezo (matajiri) ni mara nne ya matumizi ya watu maskini.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Doroth Mwanyika, akizungumzia hali ya umaskini na changamoto za MKUKUTA, anasema ingawa pato la taifa linaonekana kukua kutoka asilimia 6.4 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 6.9 mwaka 2012, bado hali ya umaskini kwa wananchi wa vijijini ni kubwa.

Kutokana na hali hiyo, anasema changamoto iliyopo ni kuhakikisha maeneo ya vijijini yanatiliwa mkazo kwa kuboresha huduma za afya, miundombinu na kubwa zaidi ni kuhakikisha sekta ya kilimo na viwanda inapewa kipaumbele.

“Ingawa nchi inaonekana uchumi wake unakua, lakini umaskini kwa wananchi wa vijijini ni mkubwa, kinachotakiwa ni kuinua sekta ya kilimo ambayo ndio inaajiri kundi kubwa la watu vijijini pia kuimarisha sekta ya viwanda”, anasema Mwanyika.

Kadhalika anasema ili kukabiliana na umaskini huo hususan kwa wananchi wa vijijini, ipo haja ya kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji ili kurahisisha kilimo. Na kwamba katika kutekeleza azma ya kuinua sekta ya kilimo bajeti ya kilimo katika mwaka wa fedha 2013/14 shilingi bilioni 7.8 zimetengwa kwa ajili ya kusaidia mfuko wa pembejeo za kilimo.

Fedha hizo zinatumika kuwapatia wakulima mikopo ya pembejeo za kilimo kama vile matrekta, power tila, zana za umwagiliaji na machine za kuongeza thamani mazao.

Vilevile, kuwapa vijana mafunzo yatakayowawezesha kujiajiri na kuhakikisha tatizo la nishati ya umeme linatengemaa, ili viwanda na sekta nyingine zinazotumia nishati hiyo ziweze kufanya kazi ipasavyo.

Hata hivyo pamoja na uwepo wa juhudi hizo bado suala la ajira nchini, ni kikwazo cha umaskini ambapo takwimu za mwaka 2001/07 zinaonesha sekta ya kilimo imeendelea kutoa ajira nyingi kwa kuajiri wananchi asilimia 77, ya Watanzania wote.

Lakini pamoja na sekta ya kilimo kutoa ajira nyingi kwa wananchi, bado mchango wake kwa pato la taifa ni mdogo wa asilimia 26, na kwamba wakulima wengi bado hawanufaiki kwenye sekta hiyo.

Kadhalika sekta ya viwanda pamoja na umuhimu wake nchini lakini haina mchango mkubwa kwenye ajira na kwamba sekta hiyo imetoa ajira kwa watu 50,000 pekee kwa mwaka 2007.

Takwimu za ajira nchini zinaonesha kuwa, wastani wa kila mwaka kuna watu 740,000 wanaoingia katika soko la ajira, wakati ajira zinazotengenezwa kwa mwaka ni 40,000 pekee.

Aidha, kwa mujibu wa matokeo hayo ya utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi nchini, hali ya nishati ya umeme vijijini ni mbaya ambapo wananchi wanaopata nishati hiyo asilimia pekee ukilinganisha na maeneo ya mijini ambayo hupata umeme kwa asilimia 36.

Hiyo ni kwamba nishati pekee au tegemezi kwa wananchi wa vijijini ni mafuta ya taa kwa ajili ya kupata mwanga na hutumia kuni kwa ajili ya matumizi ya kupikia.

Akizungumzia matokeo hayo na nini cha kufanya kuinua hali za wananchi wa vijijini, Mtakwimu Mwandamizi wa NBS, James Mbongo anasema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kutoa taarifa zinazotumika katika ukokotoaji wa mienendo ya bei za walaji nchini.

Aidha, zinasaidia kupata orodha ya bei ya bidhaa muhimu zinazotumika na wananchi wengi kwa kipindi hicho na kwamba watunga sera wanatumia takwimu hizo kutunga sera bora zinazoangalia hali ya wananchi na kutoa vipaumbele kwenye maeneo muhimu kama hayo ya vijijini.

Hivyo basi, watunga sera, wachumi na hata wadau wa masuala ya maendeleo nchini wanatakiwa kuchukua matokeo hayo na kuangalia jinsi ya kusaidia maeneo ya vijijini, ambayo bado yanakabiliwa na umaskini mkubwa, ukilinganisha na maeneo ya mijini.

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi