loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Umitashumta, Umisseta iendelezwe, ithaminiwe

Michezo hiyo iliyoshirikisha kanda 11 na jumla ya wanafunzi 15,000, ilihusisha michezo ya netiboli, soka maalumu na lile la kawaida, mpira wa mikono, wavu, riadha na goal ball ambao hushirikisha wachezaji wenye ulemavu wa macho.

Katika hotuba yake ya ufungaji, Naibu Waziri Nkamia aliwataka wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha kila shule inakuwa na viwanja vya michezo na vile vinavyotumika kulishia mifugo, vitumike kwa ajili ya kuchezea michezo.

Aidha, alisema shule nyingi hazina viwanja vya michezo na hivyo kushindwa kuendesha michezo katika shule zao, huku akibainisha kuwa michezo ya shule za msingi na ile ya sekondari ndio chimbuko kubwa la wanamichezo wengi, hivyo alitaka iendelezwe na kuviendeleza vipaji vinavyopatikana katika michezo hiyo.

Kwa mujibu wa Nkamia, kama sio michezo hiyo, wasingekuwepo baadhi ya nyota wa michezo nchini ambao walifanya vizuri huko nyuma baada ya vipaji vyao kuibuliwa na kuendelezwa kutoka katika michezo ya Umishumta na Umisseta.

Tunaungana na Naibu Waziri Nkamia kusisitiza umuhimu wa michezo hiyo ya Umitashumta na Umisseta ambayo mwaka huu ilimalizika siku chache zilizopita Kibaha kabla ya kuanza kwa ile ya Umitashumta.

Kimsingi, michezo hii ni muhimu sana katika Taifa kwani inasaidia katika kuwaandaa wanamichezo wetu wa baadaye nchini, kwani vijana hawa wanakuwa ni wenye uwezo wa kuendelezwa kwa maana ya kupatiwa mafunzo zaidi katika michezo wanayoimudu ili wawe na viwango vya juu.

Watanzania wengi kama alivyoeleza Naibu Waziri, wanafahamu jinsi michezo ya Umitashumta na ile ya Umisseta ilivyoibua wanamichezo mahiri wa Tanzania katika michezo mbalimbali na ambao katika miaka ya 1970 hadi 1980, ndio waliokuwa wakiiletea Tanzania sifa kimataifa.

Hivyo hakuna ubishi kuwa bado michezo hii inapaswa siyo tu kuendelezwa, bali kuthaminiwa kwa maana ya kuweka mkazo katika kuhakikisha kila halmashauri nchini kama siyo kila shule, inashiriki ipasavyo kuwaandaa wanamichezo wao kwa ajili ya michezo hii ya kila mwaka.

Sote tunafahamu kuwa michezo pia ina mchango mkubwa katika kujenga afya za vijana wetu, kumsaidia katika kumjenga kiakili, lakini sasa michezo imekuwa moja ya eneo linalotoa ajira kwa wingi duniani katika michezo ya aina mbalimbali, hivyo kwa wanafunzi hawa ni eneo la kujipatia ajira baada ya masomo yao.

Ni vyema basi ikatumika kama fursa ya kuwaandaa vijana hawa kwa maisha yao ya baadaye kwa kutumia vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu, na njia rahisi ya kuwasaidia ni kuviendeleza vipaji hivyo na kuhakikisha michezo ya Umitashumta na Umisseta inasimamiwa vyema na inapewa msukumo unaostahili kama sehemu ya kuibua vipaji na kuwaandaa wanamichezo wa baadaye wa Tanzania.

UCHAGUZI Mkuu wa madiwani, wabunge, wawakilishi, Rais wa Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi