loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Umoja wa Mataifa waonya vyombo vya habari

Akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari ya namna ya kuripoti habari za uchaguzi mkuu juzi mjini Bagamayo, Rodriquez alisema bila vyombo vya habari kutoa habari za huru na haki juu ya mchakato huo wa kidemokrasia, wananchi hawataweza kupata taarifa sahihi kuhusu wagombea na sera za vyama.

Alisema hii ina maana kuwa vyombo vya habari vizingatie usawa wa kijinsia na kuhakikisha mambo yote muhimu ili kuufanya uchaguzi huo unakuwa wa uwazi, wa uhakika na wa amani.

Semina hiyo iliandaliwa na Jukwaa la Wahariri (TEF) na kudhaminiwa na UNDP.

Mkurugenzi huyo mkazi alisema kwa uchaguzi wa Oktoba, vyombo vya habari vya Tanzania vinatakiwa kuepuka kutoa habari za upendeleo ili kuwapa nafasi wananchi wafanye maamuzi sahihi bila kuvutwa na ushawishi wa baadhi ya vyombo vya habari.

Lakini hata hivyo alisema pamoja na wajibu huo wa vyombo vya habari, mkurugenzi huyo aliwataka kuhakikisha katika kutoa kwao taarifa wanazingatia maslahi ya taifa na ya jamii. Alivitaka pia kutoa taarifa za kina kuanzia uandikishaji wa wapigakura hadi wakati wa kuhesabu kura na haki za wananchi katika mchakato huo wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa TEF, Absolom Kibanda, alitoa mwito kwa waandishi wa habari kuhakikisha wanafanyia kazi mambo yote ambayo yametolewa kwenye mafunzo hayo, likiwemo suala la kuhakikisha baada ya uchaguzi Watanzania wanaendelea kuwa na amani.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Shadrack Sagati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi