loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Umoja wa Ulaya wavutiwa na Kigoma

Akizungumza baada ya ziara ya siku tatu mkoani humo, kiongozi wa timu hiyo ya mabalozi katika ziara hiyo, Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi alisema kuwa miradi hiyo imeonya dhamira ya dhati katika kutekeleza mkakati wa kuondoa umasikini kwa jamii.

Katika ziara hiyo, balozi huyo alisema amevutiwa na mradi wa uboreshaji kahawa kwa kupanda miche inayohimili magonjwa na usambazwaji wa mashine za kukobolea kahawa kwa vikundi vya wakulima.

Alisema kahawa inayo nafasi kubwa ya kuwasaidia wananchi katika kuondokana na umasikini na kwamba serikali inapaswa kuweka mkakati zaidi katika kutumia zao hilo, kama moja ya njia za kuwasaidia wananchi kupambana na umasikini.

Balozi huyo aliitaka serikali ya mkoa Kigoma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kutumia Ziwa Tanganyika kama rasilimali muhimu ya kuimarisha uchumi kwa kutumia nchi zinazopakana na ziwa hilo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina yao.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya aliwaambia mabalozi hao kuwa kuimarika kwa amani katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, imetoa fursa mpya kwa mkoa huo kutumia nafasi hiyo katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi hizo.

Machibya alisema kuwa mkoa wa Kigoma kwa sasa unafunguka kwa kasi katika suala la miundombinu, jambo ambalo limevutia wawekezaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi na kuona umuhimu wa kuwekeza mkoani humo.

Miongoni mwa miradi ambayo nchi hizo za Ulaya zinafadhili ni mazingira, maliasili, ufugaji nyuki na uboreshaji kahawa kwa kupanda mbegu mpya.

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi