loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UN: Ukosefu wa ajira kwa vijana ni janga la dunia

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez. Mratibu huyo alisema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan.

Alisema ukosefu wa kazi kwa sasa ni tatizo la kijamii na kwamba, shauri hilo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuwa chanjo cha matatizo makubwa ya usalama na amani katika taifa.

Alvaro Rodriguez ambaye alifika katika ofisi za UTPC kuangalia mambo yanayofanyika katika ofisi hiyo wakati akiwa ziarani mikoa ya Kanda ya Ziwa wiki iliyopita, alisema kama tatizo la ajira litaendelea kuwapo, vijana wanaoathirika wanaweza kufikiria njia nyingine isiyo ya kistaarabu kufanikisha mambo yao.

Alisema Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali mbalimbali kuhakikisha kwamba tatizo la ajira kwa vijana linamalizwa ili jamii isiingie katika mtafaruku utakaokosesha amani na usalama na hivyo kusimamisha maendeleo yaliyofikiwa katika jamii.

Alisema makundi ya hatari mara nyingi ni ya vijana ambao wanashindwa kupata riziki au hawajui wafanye nini kupata riziki na huku wakifikiria kwamba serikali zimewaacha bila kuwaangalia.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Karsan alimwambia mratibu huyo mambo ambayo yamefanywa na umoja huo na changamoto walizokumbana nazo kwa kuzingatia mpango mkakati wake wa mwaka 2011-2013.

Umoja huo ambao ulianzishwa mwaka 1996 na kusajili na Wizara ya Mambo ya Ndani kama taasisi isiyokuwa ya kiserikali (NGO) mwaka uliofuata, umefanikiwa kuanzisha mfuko wa kusaidia vyombo vya habari kwa jina la Daudi Mwangosi, aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari wa Iringa (IPC).

Aidha alimwambia kwamba wamefanikisha mafunzo ya kuongeza umahiri wa uandishi wa habari na pia kuwaelezea umma juu ya uhuru wa vyombo vya habari.

Alisema hata hivyo bado wanaendelea na kampeni yao kutaka mabadiliko ya malipo kwa waandishi wa habari wanaojitegemea ambao ndio wanatoa mchango wa asilimia 75 hadi 80 za habari zinazotangazwa au kuchapishwa.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi