loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Upelelezi kesi ya Che Mundugwao wakamilika

Madai hayo yalibainishwa jana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo. Kweka aliiomba mahakama kuahirisha mara moja kabla ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo ya awali.

Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo mpaka Novemba 18, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa walirudishwa rumande.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni mwanafunzi Ahsan Ali Iqbal au Ali Patel, raia wa Uingereza, ofisa ugavi wa Idara ya Uhamiaji, Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, mfanyabiashara Ally Jabir, Rajab Momba, Haji Mshamu, Adam Athuman na Abdallah Salum.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 11 ya kula njama za kutenda kosa, wizi wa hati 26 za kusafiria zenye thamani ya Sh milioni 1.3 mali ya serikali, kughushi hati za kusafiria, kukutwa wakimiliki hati zaidi ya moja.

Che Mundugwao na wenzake wanaendelea kusota rumande kutokana na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwasilisha hati ya kupinga dhamana yao.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi