loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Upelelezi mauaji ya Dk Mvungi bado

Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Emilius Mchauru.

Hata hivyo Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 2 mwakani itakapotajwa tena kwa kuwa Hakimu Mkazi Sundi Fimbo anayesikiliza kesi hakuwepo.

Washitakiwa hao ni Chibago Magozi (32), John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Longishu Losingo (29) mlinzi, Masunga Msukuma (40), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40) , Zacharia Msese (33) Msigwa Matonya (30), na Ahmad Kitabu (30).

Wanadaiwa Novemba 3 mwaka huu, katika eneo la Msakuzi Kiswegere walimuua Dk. Edmund Mvungi kwa kukusudia.

Washitakiwa hao wataendelea kusota rumande kwa kuwa kesi inayowakabili haina dhamana. Hivi karibuni washitakiwa hao waliomba watenganishwe gereza kwa kuwa wanapigana na kutishiana kuuana.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi