loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ushahidi mabomu ya Arusha watakiwa

Pinda alimtaka mbunge huyo, kuwasilisha tuhuma hizo baada ya Nassari kudai kuwa anao ushahidi kuwa mtuhumiwa huyo (hakumtaja), aliteswa vibaya na jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kumhamisha magereza mbalimbali na kulazimishwa amtaje Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, kuwa ndiye aliyehusika na tukio hilo.

Katika swali lake kwa Waziri Mkuu, alitaka kujua kama vyombo vya dola kazi yake ni kubambikia watu ili kuwadhibiti viongozi wa upinzani hususani wa Chadema.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema si rahisi kwake swali hilo kwa wakati huo kwa kuwa tayari mbunge huyo ameonesha kuwa na taarifa zote, hivyo ni vyema aziwasilishe zifanyiwe kazi ili ibainike kama ni ukweli au la.

“Suala lile la kulipua bomu Olasiti na baadaye Uwanja wa Soweto halikuwa jambo dogo hata kidogo, presha kubwa ya watu wanataka kujua nani alilipua, kwanini na akinanani wanahusika,” alisema Pinda.

Alisema maelezo aliyoyatoa Nassari hayafamu, hivyo ni vyema mbunge ayaandike kwa kina na kumpatia Waziri anayehusika, ili afuatilie tuhuma kwa tuhuma na kubainisha kote kulipokosewa na kurekebisha.

Baada ya jibu hilo, nje ya Ukumbi wa Bunge kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Almas Apollo, mkazi wa Nzega ameibuka na kudai aliteswa na Polisi na kulazimishwa kusema alihusika katika mlipuko wa bomu hilo akishirikiana na Lema.

Apollo alidai yeye ni mzaliwa wa Nzega na mwaka 2010 alikamatwa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutumia silaha na kupora dhahabu Mwanza.

Alidai alipelekwa Mwanza na kukaa kwa siku saba na baadaye Geita alipokaa siku 14 kwa tuhuma za wizi wa silaha na kufunguliwa kesi tatu na baada ya siku nne aliondolewa kesi mbili na kubaki moja ya unyang’anyi kwa kutumia silaha na kufungwa miaka 30 kuanzia Oktoba 2011.

Kijana huyo alidai tangu muda huo alikuwa jela ambapo alikata rufaa mpaka Mei 20 mwaka huu, alipoachiwa huru na kwenda kwao Nzega.

Alidai Agosti 5 mwaka huu alikamatwa na mwenzake Bernad John ambaye walibambikizwa mabomu mawili na kudaiwa wamekamatwa wakiwa na mabomu.

Kwa mujibu wa madai ya kijana huyo, alipelekwa Arusha na kuambiwa anahusika na ulipuaji mabomu mkoani hapo na kuelezwa ili suala hilo liwe rahisi, afuate wanachotaka wao amtaje Lema kuwa anaratibu masuala ya mabomu kwa kumtumia yeye na mtu anayeitwa Kamau ambaye ni raia wa Kenya.

Alidai baada ya hapo alipelekwa kuhojiwa kwa mtu waliyemuita Kamishna wa Kikosi Maalum na ndipo aliwaeleza kuwa mabomu yalilipuliwa wakati akitumikia kifungo Uyui mkoani Tabora, ndipo alirudishwa Nzega na kushtakiwa kwa tuhuma za kupatikana na mabomu Nzega wakati kwingine kote alikuwa akituhumiwa kwa mauaji Arusha.

“Kesi iliendelea mpaka Desemba 16 nilipopata dhamana na nikasikia Lema akichangia kuhusu mabomu nikajiuliza nitampataje ndipo niliunganishwa na Lema,” alidai.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi