loader
Picha

Ushirikiano wa MC, watoa huduma nguzo ya ufanisi

Suala lenyewe ni MC kushirikiana na watoa huduma wengine katika shughuli ili kuongeza hamasa na furaha kama shughuli husika ni ya furaha.

Hata kama ni ya huzuni kama msiba, bado ushirikiano huu unahitajika. Kwa leo nazungumzia upande wa shughuli za furaha kama harusi, kuagwa binti, kufundwa binti, kumtoa mtoto ndani na sherehe nyingine zote za kidini na kijamii.

Inapendeza sana kushauriana na wakongwe katika huduma hizi kwamba, ushirikiano wa watoa huduma katika shughuli hufanya kazi iwe nyepesi na nzuri ya kupendeza.

Kwa mfano, MC ni vyema ukawafahamu mapema wanaohudumia chakula, picha, watu wa mapambo, usafiri kama ni kampuni na watoa huduma wengine kama si wa kampuni yako wewe MC, lazima uwafahamu.

Uliza majina ya kampuni zao, wanakopatikana, mawasiliano yao, kama kuna matukio makubwa ambayo wamewahi kutoa huduma, mfano Bungeni, katika ofisi za wizara mbalimbali, kwenye sherehe kubwa au misiba mikubwa iliyoigusa jamii kwa upana.

Hii inasaidia kuonesha kuwa watoa huduma wapo pamoja na kuongeza kazi kwao maana MC ndio muongozaji wa shughuli, yaani ndio nahodha, na dereva katika shughuli.

Ushirikiano katika shughuli unaongeza ufanisi wa MC katika kufanya kazi vizuri na yenye ubora mkubwa zaidi ya kufanya kazi bila kuwajua watoa huduma wenzako katia shughuli husika.

Hivyo nakukumbusha MC mwenzangu hakikisha ukifika kwenye shughuli, ulizia watoa huduma wenzako na pia kwa kufanya hivyo unaongeza wigo wa kufanya kazi pamoja na mnajenga familia moja hata mkikutana kwenye kazi nyingine inakuwa rahisi sana maana vionjo vyako wanavifahamu na wewe unavifahamu vya kwao.

HIVI karibuni Wizara ya Nchi Ofi ...

foto
Mwandishi: Na MC GloTe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi