loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usilazimishwe kufanya kazi usiyoipenda

Niliwasiliana naye kwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) kuhusu suala la kazi na kusoma, na amenieleza kuwa, ameacha kazi aliyokuwa akiifanya hotelini kwa kuwa ametofautiana na bosi wake na anapanga kwenda kusomea Ualimu.

Nilimdadisi msichana mwenye miaka 20 kama anakwenda kusoma ualimu kwa sababu ni kazi anayoipenda au la, jibu lake ni msingi wa hoja yangu leo.

Anasema, yeye hapendi kuwa mwalimu ila ataifanya kazi hiyo kwa kuwa baba yake mzazi anataka hivyo. Alichoniambia kilinikera na alifahamu hivyo.

Msichana huyo anawawakilisha watu wengi kutoka kwenye familia tofauti waliosomea au wanaosomea fani/taaluma fulani si kwa sababu wanazipenda ila walilazimishwa na wazazi wao.

Kuna watu ni walimu, madaktari, wanajeshi, polisi nk, leo si kwa sababu wanazipenda kazi hizo, walikwenda huko kutekeleza matakwa ya wazazi wao.

Kumlazimisha mtoto awe daktari wakati yeye anapenda kuwa mhandisi ni unyanyasaji, uonevu na ukatili unaoweza kusababisha mtu ajute na kunung’unika kwa kipindi kirefu cha maisha yake.

Mimi nafanya kazi ninayoipenda na si kwa sababu ya wazazi wangu au mtu mwingine alipenda iwe hivyo, niliamua mimi.

Nilimuuliza yule msichana wa Mwanza kwa nini uwe mwalimu wakati ni kazi usiyoipenda? Utakapopata matatizo huko ya kikazi utamlaumu baba au utajilaumu wewe?

Nilimwambia“Kama unapenda kuwa mwalimu its ok kasome, kama hupendi acha, fanya kazi unayoipenda wewe, kazi utafanya wewe hatafanya baba, kazi ni kama mume au mke, utaishi naye wewe…ndoa na kazi ndiyo maisha yako, tumia busara kuamua.”

Ninaamini nipo sahihi kuamini kwamba, kijana anapaswa kuwa huru kuchagua afanye kazi ipi katika maisha yake, ushauri wa wengine wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa na marafiki ruksa lakini yeye awe na uamuzi wa mwisho.

Kijana ni mtu mzima na ana utashi, ashauriwe na kuwezeshwa kuboresha kile alichokichagua yeye na si kumlazimisha afanye kazi ambayo yeye haipendi.

Baba na mama yangu ni wazazi wangu, wana nafasi yao katika maisha yangu hasa ushauri, ila hawana mamlaka ya kuamua nisome fani ipi au nifanye kazi gani.

Wazazi wanapaswa kuheshimu hisia za watoto wao, wawasaidie kugundua na kuviendeleza vipaji vyao, na wasichoke kuwa washauri kwa kuzingatia uzoefu wa kule walikopita wao. Siku njema. bmsongo@hotmail.com

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi