loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Utekelezaji matumizi ya EFD una kasoro’

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Chalinze wilayani Bagamoyo, Kinana alisema kuwa hana matatizo na uamuzi wa kutumia mashine hizo bali ana matatizo na utaratibu uliotumika katika kuanzisha matumizi yake.

“Naomba waandishi wa habari mnielewe vizuri katika hili. Sina matatizo na uamuzi wa kutumia hizi mashine, lakini utaratibu wa kuzitumia ndio una matatizo na hilo si sawa,” alisema Kinana wakati akihutubia mkutano huo.

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Pwani, Kinana alisema katika maeneo yote aliyopita kumekuwapo malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambayo aliyasema ni ya msingi na yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi.

Kinana alibainisha kasoro hizo kuwa ni gharama ya kununua mashine hizo ambayo awali wafanyabiashara waliuziwa kwa Sh milioni nne na baada ya kuibuka malalamiko mengi bei yake imepunguza hadi kufika Sh 600,000.

Mamlaka ya Mapato (TRA) inawataka wafanyabiashara kuzinunua mashine hizo na watarudishiwa fedha zao kidogo kidogo kama makato pungufu katika kodi wanazolipa.

Hata hivyo, Kinana alihoji nani atarejesha fedha au kufidia hasara itakayopatikana kutokana na fedha zilizotumika kununua mashine hizo pindi mfanyabiashara atakapofilisika kabla ya kulipwa deni.

Kinana alisema kuwa ugumu wa utekelezaji wa matumizi ya EFD unatokana na matatizo katika sheria inayohusu matumizi ya mashine hizo na kuwa wafanyabiashara wanaopinga wasionekane kama ni wakorofi.

Tangu kuanzishwa kwa matumizi ya EFD miezi ya hivi karibuni kumekuwa na malumbano baina ya wafanyabiashara na TRA baada ya wafanyabiashara kuhoji na kugomea utaratibu wa matumizi yake katika maeneo mbalimbali ya nchi.

WASTANI wa bei za nafaka katika masoko mbalimbali nchini zimepungua ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi