loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UTT yajikita kuipa thamani ardhi

UTT ni kampuni ya Serikali ambayo imejikita katika kuongeza thamani ya ardhi, kwa kupima na kuweka miundombinu mbalimbali ikiwamo ya maji, umeme na barabara ili kuongeza thamani yake.

Tangu Julai mwaka huu, imeamua kuanzisha mkakati wa kuboresha ardhi ambayo ama ilikuwa haiendelezwi au haikuwa na thamani kubwa kutokana na kutokuwa na miundombinu muhimu inayostahili. Miongoni mwa miradi maarufu nchini ni kuongeza thamani ardhi upo Mapinga, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Katika mradi huo, UTT imenunua ardhi kutoka kwa kampuni ya Apex na kuamua kuiboresha na kuiwekea miundombinu. Meneja Mradi huo, Godfrey Mwakabole, anasema mradi wa Mapinga ni miongoni mwa miradi nchini ambayo taasisi yake inaamua kufufua ardhi au miradi iliyolala.

Kampuni hiyo ya Serikali, imebaini mahitaji halisi ya watu, kukosa fedha za kuipa thamani ardhi na hiyo imeamua kuipa thamani. Miradi mingine kama hiyo inatekelezwa katika miji ya Bukoba, Lindi na Mtwara na maeneo mengine ya Sengerema na Mombo ambao unafanyika upembuzi yakinifu.

Mwakabole anasema, eneo hilo halikuwa linaendelezwa kwa miaka mingi, Kampuni yake imenunua na kuiwekea miundombinu. Miundombinu iliyopo ni pamoja na maji, umeme, upimaji viwanja na utengenezaji barabara za kati ya viwanja. Kampuni hiyo inapima viwanja takribani 1,000 kwa ajili ya matumizi ya watu mbalimbali ajili ya makazi na huduma nyingine muhimu za maendeleo kama shule, zahanati, viwanja vya michezo na maeneo ya kuabudia.

Katika awamu ya kwanza ya mradi viwanja 246 vimeshapimwa na takribani shilingi bilioni tatu zinatumika kwa ajili ya kuingiza miundombinu ya maji, barabara, umeme na mtaalamu mshauri kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji eneo hilo.

Tayari tangi la maji linajengwa kwenye viwanja hivyo na lengo lake ni kuhakikisha kwamba wakazi wa eneo hilo, wakikosa maji ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), watatumia maji ya kwenye tangi hilo.

Kutokana na kuipa thamani ardhi hiyo, inageuka kuwa makazi bora kwa ajili ya wakazi, taasisi na kampuni ambazo zinataka kutumia ardhi hiyo mara baada ya kuongeza thamani. Katika kuipa thamani ardhi hiyo, UTT imeingia mkataba na kampuni ya SIECO ambayo ndiyo inatengeneza barabara zinazopita kwenye viwanja ambayo inasaidia katika kuboresha viwanja na kuvipa thamani kubwa.

Kampuni hiyo ndiyo pia inashughulika na kuingiza maji kwenye tangi kubwa lenye uwezo wa lita 1,500 katika eneo hiyo. Tangi hilo ni muhimu katika kumaliza tatizo la maji katika eneo hilo. UTT imeingia makubaliano na kampuni ya umeme ya Kim, ambayo inashughulika na kuingiza umeme katika eneo hilo ambalo sasa limepanda thamani baada ya kuingiza miundombinu hiyo.

Mshauri Mtaalamu Kampuni ya Nimeta nayo imeingia mkataba na UTT, anahakikisha kwamba mradi huo unafanikiwa kutokana na kuwepo miundombinu muhimu katika kuboresha makazi ya watu na huduma nyingine. Kampuni hizo zinasaidia kuboresha ardhi, ambapo katika awamu ya kwanza ya viwanja 246, kati yake viwanja 70 wamegawiwa wananchi waliopenda makazi hayo yaliyoboreshwa.

Viwanja hivyo baada ya kuboreshwa miundombinu vinavyouzwa Sh 25,000 kwa meta za mraba. Mwakabole anasema, kampuni yake imewapa wanunuzi wa viwanja mwezi mmoja hadi Novemba 30 lakini unaweza kuongezwa kutokana na mnunuzi kuonesha nia na malipo yanalipwa kupitia benki ya Posta.

Kampuni yake imewapa ruhusa wanapenda viwanja hivyo kwenda kuangalia mara baada ya kuweka rehani shilingi milioni moja, ambavyo wakishalipa fedha zao hatimiliki zitabadilishwa kutoka kampuni hiyo hadi majina ya mmiliki binafsi. UTT inashughulikia na kuandaa mazingira hayo kwa kufyeka nyasi ili kuonesha vipimo vya viwanja kutoka kimoja hadi kingine, ili wamiliki wakinunue waone na kujua mipaka yao.

Mwakabole anasema, awamu ya pili ya mradi huo, viwanja na utahuisha ujenzi wa nyumba katika viwanja 254. Nyumba hizo zitaandaliwa ramani za aina 15, ambazo wateja wanaotaka viwanja hivyo watajenga kwa kutumia ramani hizo. Katika awamu hiyo, mnunuzi atanunua kiwanja na kuchagua ramani kwa ajili ya kujenga nyumba katika eneo husika.

Mtu hafungwi kuchagua ramani ya mwenzake. Wanunuzi wanaweza kwenda kwenye taasisi za fedha kuomba mikopo ili kununua viwanja na kujengewa nyumba kadiri ya ramani hizo. Benki zinazotaka kusaidia watu wanaotaka kujenga makazi bora na ya kisasa, zinakaribishwa na huu ndio wakati muafaka kuwakopesha watu wenye nia kuomba mikopo kujenga makazi katika eneo hilo la ufukweni.

Mradi huo wa viwanja 1,000 ni msaada mkubwa kwa wenyeji wa eneo hilo kwani watapata huduma mbalimbali zikiwamo za maji, barabara na huduma nyingine kutoka kwenye makazi hayo bora. Jambo muhimu katika makazi hayo ni matumizi na utunzaji wa miundombinu, mtindo ambao Kenya wamesonga mbele na UTT imeamua kutumia mbinu ambazo wanatumia katika kuhifadhi na kutunza makazi hayo.

Johnson Mwangi, kutoka Kenya wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Home Liberty, ameelekeza baadhi ya wanunuzi wa eneo hilo, namna ya kutumia miundombinu na kuitunza. Mwangi anasema, wakazi wa eneo hilo, wanatakiwa kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kutumia miundombinu ikiwamo ya kusafirisha barabara, kujenga mabomba ya kuingiza maji kwenye nyumba na matumizi mengine.

Makazi hayo yanahitaji usafi, hiyo wakazi wa eneo wanahitaji kulipia gharama mbalimbali zikiwamo za taa za barabarani, ulinzi maeneo na miundombinu kuzunguka makazi hayo. Wakazi wa eneo wanatakiwa kutumia rasilimali hizo za umma kwa uangalifu na kuzilinda kwa nguvu zote, zitadumu kwa muda mrefu na kubaki kuwa bora pamoja na makazi kwa muda mrefu.

Kampuni hiyo imeweka malengo ya kuendelea kuboresha ardhi katika maeneo mbalimbali. Mkakati huo, unahusisha pia ardhi ya watu binafsi ambayo inaweza kuwa mahali pazuri na panapoweza kuleta faida kwa kampuni.

UTT ilianza rasmi mwaka 2003, hadi Julai 2013, imegawanyika katika kampuni tatu, ya kwanza ni inayojishughulisha na fedha, raslimali; ya pili inajishughulisha na huduma za vitega uchumi vikiwamo vipande vya umoja, na ya tatu ni hii ya uendelezaji miradi na miundombinu.

“MTU niliyefanya naye mahojiano alikuwa anafanya kazi kwenye ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi