loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uturuki yaanza kulipa Yanga

Kwa ushindi huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabingwa hao watetezi wameendelea kukaa kileleni kwa kufikisha pointi 31, ikifuatiwa kwa karibu na Azam FC na Mbeya City ambazo pia jana zilionja ladha ya ushindi katika mechi zao za kwanza za mzunguko huo.

Mabao ya Yanga iliyokuwa chini ya makocha wapya, Mholanzi Johannes van der Pluijm na mzawa, Charles Boniface Mkwasa, yalifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 52 na David Luhende dakika ya 80.

Timu zote zilianza mchezo kwa kushambuliana na kupoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga, huku Yanga ikipoteza nafasi tatu kupitia kwa Kavumbagu, Said Bahanuzi na Mrisho Ngassa. Kavumbagu alibaki yeye na kipa, lakini badala ya kufunga, alitaka kumpiga chenga, lakini kipa huyo wa Ashanti United, Daudi Mwasonge aliokoa hatari hiyo.

Ashanti wakiwa chini ya Kocha mpya, Abdallah Kibadeni aliyetupiwa virago na Simba, walionekana kuchangamka, huku mchezaji wake, Bright Obinna akipoteza nafasi ya wazi ya kufunga baada ya kumpiga chenga beki Juma Abdul wa Yanga.

Dakika ya 37, Yanga ilimtoa Bahanuzi na nafasi yake kuchukuliwa na Simon Msuva na Haruna Niyonzima alikosa nafasi ya wazi ya kufunga eneo la hatari baada ya shuti kale kupaa. Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Yanga walikianza kwa kasi na walipata bao la kwanza katika dakika ya 52, likifungwa na Kavumbagu akiunganisha pasi ya Simon Msuva.

Baada ya kuingia kwa bao hilo, Ashanti walijitahidi kulishambulia lango la Yanga na wakapata bao la kusawazisha dakika ya 61 likifungwa na Obinna aliyemalizia kazi nzuri ya Hussein Sued.

Wakati mchezo huo ukitazamiwa kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Luhende aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 80 na kuihakikishia pointi zote tatu. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga iliwachapa vijana hao wa Ilala mabao 5-1.

Kwa upande wake, Azam FC na Mbeya City zimeendelea kuifukuzia Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya vijana wa Chamazi, kuizamisha Mtibwa Sugar kwa bao 1-0, sawa na Mbeya City iliyopata ushindi kama huo ugenini Kaitaba mjini Bukoba dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.

Bao la Azam lilifungwa na Kipre Tchetche kutokana na pasi iliyopigwa na Joseph Kimwaga, na kuwachomoka mabeki wa Mtibwa na kufumua shuti lililojaa moja kwa moja wavuni.

Bao la Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar lilifungwa na Richard Peter dakika ya 72. Mjini Tanga, Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Oljoro, wakati leo Simba chini ya kocha mpya, Zdravko Logarusic inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mgambo Shooting ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Complex.

KOCHA wa timu ya taifa, ‘Taifa ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi