loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uvamizi mgodi wa Nyamongo utafutiwe dawa

Tukio kama hilo limejirudia Ijumaa ambapo safari hii kwa mtindo ule ule, aliuawa mtu mmoja baada ya kukabiliana na polisi wanaolinda mgodi huo waliolazimika kufyatua risasi baada ya kukaribia kuzidiwa nguvu na kundi la raia wapatao 100.

Matukio haya mawili ni ya kusikitisha na mara zote yanaiweka nchi katika taswira mbaya, na hata wakati mwingine wanaharakati wa haki za binadamu kuibatiza kuwa ni nchi isiyozingatia haki za binadamu. Tunaipa pole familia ya Daniel Masimbe, ambaye aliuawa kwa risasi katika mapambano na polisi hao na kumwombea roho yake ilazwe mahali pema peponi, lakini pia akiwa ameacha hadhari kwa wananchi waliosalia.

Tunaelewa kuwa kinachowasukuma wananchi hao kuvamia mgodi huo ili kujipatia mchanga na au mawe, ni umasikini ingawa pia kunawezekana kukawa na mashinikizo mengine ya kiuanaharakati na hata kisiasa.

Lakini itoshe tu, kusema kuwa hatua ya wananchi kuchukua silaha za jadi na kuvamia mgodi wa mwekezaji ambaye naye analinda raslimali zake ambazo amemilikishwa kihalali si tu ni uchokozi, lakini pia ni hatari kwa maisha kama ambavyo tumeshuhudia mara mbili damu ikimwagika.

Ni wazi kuwa kuna upande utalalamika kwamba polisi wanachukua sheria mkononi kwa kutumia vibaya dhamana waliyopewa ya kulinda usalama wa raia, lakini pia ieleweke, kuwa nao wanalinda mali za raia hao hao.

Kwa sasa mgodi wa Nyamongo unamilikiwa na kampuni ya Barrick ambayo ina haki zote za kulinda mali zilizomo kwa mujibu wa mkataba, hivyo kama inaonekana hatari ya mgodi kuvamiwa na kuporwa, bila shaka mwekezaji ana haki ya kuchukua hatua.

Na hatua zinazokubalika ni kukabiliana na wahalifu na kuwakamata iwapo watakubali kukamatwa bila shuruti, lakini kama watakuja kishari na polisi kuona wanazidiwa, bila shaka nguvu za ziada zitatumika na matokeo yake huwa si mazuri.

Tunashuhudia kupoteza maisha kwa Masimbe bila shaka kutokana na kukaidi kutii amri ya polisi ambao wapo hapo kihalali kulinda raia na mali zao na kama waliona wanazidiwa nguvu na hakuna jinsi ya kukabili hali hiyo ila kutumia risasi za moto, bila shaka ndicho walichokifanya.

Hatuungi mkono polisi kuua raia, lakini pia hatuungi mkono raia kujichukulia sheria mkononi na kutaka kupora kisichohalali yao na kutumia maguvu na ukaidi hata pale wanapohadharishwa na Polisi kuacha kufanya walivyokusudia. Sisi tunawaomba wananchi wa Tarime kuacha kujiingiza katika matatizo kwa kuvamia migodi au mali zozote za wawekezaji au watu wengine kinyume cha sheria, kwani kila mtu ana haki ya kujilinda na kulinda kilicho chake.

Tunawaomba pia viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, wanaharakati na wadau wengine wa maendeleo, kuelimisha wananchi ubaya wa uhalifu lakini pia wabuni vyanzo vingine vya mapato, kuliko uvamizi ambao unawasababishia mauti na vilema vya maisha.

Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi