loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UVCCM- Vijana Arusha acheni vurugu

Aidha, umoja huo pia umesema milipuko ya mabomu jijini hapa inafanywa na vijana, kwani watuhumiwa 17 wanaodhaniwa kuhusika na matukio ya ulipuaji wa mabomu hayo, wengi wao ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 18-25.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Leguruki katika mkutano wake wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya kata hiyo.

Mapunda ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku mbili, alisema ulipuaji huo wa mabomu, unadhihirisha wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa na maadili kwa vijana, hali inayochangia wengi wao kujihusisha na vitendo viovu, vinavyoleta athari kwa jiji hilo na Taifa.

“Viongozi wa dini, wazee wa mila na wazazi naomba tuungane kwa pamoja kukemea na kuwaonya vijana wa Jiji hili kuacha mara moja tabia ya kujihusisha na vitendo viovu, ambavyo vinapoteza heshima ya jina la ‘Geneva ya Afrika’ tulilopewa, kutokana na amani upendo na mshikamo wa mkoa huu,” alisema Mapunda.

Alisema vurugu hizo, zinaathiri sekta ya utalii, ambayo inachangia uchumi wa Arusha na taifa kwa jumla.

Alisema wadau wakubwa wa sekta hiyo ni vijana, lakini hawaoni umuhimu wa kutunza amani katika mkoa huo.

Mapunda alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana, kuacha tabia ya kuwakaribisha wageni kutoka nchi za jirani kinyume cha sheria kwa kuhongwa na kuishi nao, bila kutoa taarifa kwa vyombo husika.

Alisema wageni hao huwafundisha vijana vitendo vya kigaidi.

SIKU zinahesabika ndani ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi