loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UVCCM waapa kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Sahaka katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Kuu ya UVCCM Maisara Mjini Unguja jana.

Shaka alisema vijana wa UVCCM ni Mapinduzi ya ukombozi wa umma, ambayo yalifanikiwa kufuta matabaka, ubaguzi uliofanyika bila ya huruma na ukoloni wa Kisultan kwa miaka 160 katika visiwa vya Unguja na Pemba.

“UVCCM itaendelea kuyalinda na kuyaenzi Mapinduizi hayo huku tukiwatahadharisha wapinga Mapinduzi kutambua kuwa wananchi wa Zanzibar hawatakubali kamwe kulegeza kamba ya kuyaheshimu mapinduzi yalioleta ukombozi kwa wanyonge,” alisema.

Aliwaeleza wazi maadui wa Mapinduzi walioko ndani na nje ya visiwa kuwa bado Wazanzibari wako makini usiku na mchana, na hakuna anayekubali kuutupa na kuupoteza utu na urithi wao.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisema tangu mwaka 1964 kulikuwa na mabaki ya mamluki na vibaraka waliobakia Zanzibar na kusema wasijidanganye, kujipa moyo na kufikiria kama wana ubavu wa kuyafuta Mapinduzi hayo.

Shaka alisema kwamba majina ya wana Mapinduzi wa Zanzibar chini ya Jemedari Mkuu wa Mapinduzi hayo hayati Mzee Abeid Amani Karume yatabaki kuwa ni alama na nembo ya kukishamirisha kizazi kipya ili kutambua msingi wa harakati hizo zilivyoanza na matokeo yake.

UVCCM watafanya matembezi ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi yatakayozinduliwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Micheweni Pemba Desemba 22, mwaka huu na kufungwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Jakaya Kikwete katika viwanja vya Maisara Suleiman Januari 5, mwakani kisiwani Unguja.

RAIS John Pombe Magufuli anaongoza kwenye ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi