loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

VETA wataja vyuo vinavyostahili kutoa mafunzo

“Wapo baadhi ya watu wenye uchu wa kupata fedha, wanaanzisha na kutoa mafunzo ya aina hii kinyemela. Tunazo taarifa kutoka kwa baadhi ya wazazi na wanafunzi waliokutana na utapeli huo,” alisema.

Alisema ili wazazi na wafunzi wasiingie katika mtego wa kupoteza fedha zao ni muhimu wanapojisajili katika vyuo hivyo wakazingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiridhisha na usajili wa vyuo hivyo.

“VETA ilifuta usajili wa vyuo vyote mwaka 2009 na mwaka 2010 ikafanya ukaguzi kwa vyuo vyote ili kujiridhisha kama vinakidhi vigezo,” alisema.

Alisema mwaka huu VETA ilianza kutoa vyeti vya usajili kwa vyuo ambavyo vinasifa ya kuitwa vyuo vya ufundi na vyuo vya kutoa mafunzo ya hoteli na utalii katika mikoa yote nchini.

Mgani aliwataka wamiliki wa vyuo ambavyo havijasajiliwa kufuata taratibu za kisheria ili viweze kusajiliwa ili kuepuka kufungiwa.

Alivitaja vyuo vilivyosajiliwa kuwa ni pamoja na Mufindi VTC, Ifunda Technical Secondary School , Mgongo Catholic VTC, Amani VTC, Mafinga Secretarial College, Nyabula VTC, KIlolo VTC, Isimani VTC, Sanaa House VTC, Matumaini Centre VTC, Incoment VTC, Mafinga Lutheran VTC, Kibidula Agriculture VTC, na Ifunda Mission VTC.

Vingine ni Cory Training College, Ilula Institute of Technology and Business Studies , Starcom Hotel Academy ,Ruaha Tourism College , Southern College of Tanzania , Tabez VTC, Ng'ingula VTC, ST. Jerome VTC, Ulete VTC, Upendo VTC, ST.

Therese VTC,ST Maria Goreett VTC, SCim Brothers VTC, Nyota ya Asubuhi VTC na Don Bosco Youth Training Centre.

RAIS John Magufuli ameagiza utoroshaji wa magogo kwenda nje na ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi