loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vigogo wa habari wakutana Ethiopia

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mtendaji vwa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga kwa vyombo vya habari, ilisema mkutano huo wa siku mbili unajadili masuala muhimu yanayoikabili tasnia hiyo.

“Unajadili masuala hayo na kuja na mikakati ya kuhakikisha tasnia ya habari inatekeleza dhima yake chanya katika bara hili ambalo linapitia katika mabadiliko kwa kasi,” ilisema taarifa.

Wazungumzaji mbalimbali wanajadili masuala muhimu ya kimiundombinu na kitaasisi ya kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha tasnia hiyo barani humo. Mukajanga ni mmoja wa wazungumzaji wakuu.

Mkutano huo wa mwaka huu ni muhimu hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali barani humo katika maeneo yanayohusu ubunifu wa kidijitali, uongozi na maadili pamoja na mbinu za kibiashara zinazoibuka hivi sasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kesho jopo maalumu litakaa kujadili ‘Utendaji na Changamoto za Uhuru wa Habari Afrika: Mifano ikitoka Ethiopia, Kenya, Mali, Afrika Kusini na Tanzania’.

“Uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ni viambato muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na Bara tulivu, lenye mabadiliko na linalokua. Viongozi wa tasnia ya habari katika Afrika ndio watakaochangia mjadala huu kwa uwazi jijini Addis,” alisema Amadou Mahtar Ba, ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Tasnia ya Habari katika Afrika (AMI), mwandaaji wa mkutano huo.

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uthubutu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi