loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijana: Oa, olewa ukiwa tayari kufungwa

Maisha ni haya haya uliyoishi jana, unayoishi leo, na utakayoishi kesho, kila dakika ina thamani kubwa sana, itumie vizuri leo ili kuepuka majuto kesho. Hivi karibuni nilisema, unapoufurahia ujana leo, kumbuka kuna uzee kesho.

Pole kama unataabika kwa vyovyote vile, hongera kama unakula ‘bata’, kama una familia ithamini, muheshimu mwenzi wako, mchepuko si dili, kama kweli unampenda utamlinda, Mungu hapendi tuangamie lakini hapati hasara tukifa.

Hivi sasa kuna mapinduzi kwenye suala la kuchepuka, zamani jamii iliamini kuwa jukumu la kumpangishia nyumba mwanamke ni la mwanamume, lakini sasa hali ni tofauti.

Wanawake matajiri nchini Kenya walioolewa wanawapangishia nyumba wapenzi wao a.k.a, mpango wa kando,a.k.a nyumba ndogo,a.k.a ving’asti, na kwamba, sasa wameachana na ule utaratibu wa kukutana nao gesti au hotelini.

Hapa Tanzania ni kawaida kwa mwanamume aliyeoa kumpangishia nyumba mpenzi wake (nyumba ndogo) lakini Kenya hali ni tofauti, sasa wanaume hasa vijana wanapangiwa nyumba na ‘mashugamami’ hivyo jukumu la msingi la wanaume hao a.k.a Mariyoo ni kuwatimizia wanawake hao mahitaji yao hasa kuwaridhisha kingono.

Wanasema ndoa ni pingu za maisha, bila shaka wakimaanisha kuwa, ukioa au kuolewa ni sawa na kuwa kifungoni, na kwa maana nyingine, kuoa au kuolewa ni uamuzi wa hiyari wa mtu kupoteza sehemu ya uhuru wake.

Si hivyo tu, pengine kutokana na ongezeko la talaka, kuna wanaosema kuwa, zamani watu walioana ili waishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe, lakini sasa watu wanafunga ndoa ili waachane.

Wanasema, kuoa au kuolewa ni sawa na kwenda mgahawani ukaagiza chakula lakini baada ya kuletewa unaona chakula alichoagiza mtu mwingine ni kizuri au kitamu zaidi. Hivi sasa ndoa si taasisi salama, idadi kubwa ya watu waliombukizwa Ukimwi ni wanandoa.

Mapenzi yamejaa usanii na unafiki, watu wanaigiza kupenda, wanatenda wasiyosema, na wanasema wasiyotenda, ukichepuka watu hawashangai, pengine watakuuliza tu una michepuko mingapi? Siku njema, bmsongo@hotmail.com

UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi