loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

VIJANA: Wiki ya Mhenga na Rooney imepita

Wahenga juma hili wametamba sana katika kila kona jambo lililopelekea gazeti hili toleo lake la juzi, kutoa maana halisi la neno hilo ‘mhenga’ bila shaka kwa wale ambao walikuwa hawafahamu maana sasa wamejua maana licha ya kuwa Wahenga walisema ‘Asiye jua maana usimwambie maana’ lakini habarileo limetoa maana.

Mhenga ni mtu mwenye hekima na busara, aghalabu huwa na umri mkubwa. Lakini hivi hadi uje kuwa na busara huko baadae ni lazima uwe umezifanyia maanadalizi hivi sasa. Kijana wa sasa ni mzee mtarajiwa.

Kwa tafsiri ya haraka kila mtu ni Mhenga ila tu inategemea yupo na nani. Kama una miaka 18 na upo na watoto wa miaka 12 – 15 wewe ni Muhenga, ukiwa na miaka 40 na upo na vijana wa miaka 20-30 wewe ni Muhenga wao.

Sasa unatakiwa uwe na hekima na busara. Enzi za utoto wetu miaka ya 70 huko hadi miaka ya 80 mwishoni tulikuwa tukiwaona babu zetu na bibi zetu kuwa ni watu wenye busara na wenye kujua mambo mengi sana ya dunia hii, hivyo ilitufanya kujenga mazingira watoto mtaani kujikusanya kwa babu nyakati za jioni wakati akiota moto na sisi kumsogezea kuni naye akitupa maneno ya busara na hadithi za za ujana wao.

Maneno hayo ndio baade na sisi tulikuwa tukiyasema kuwa ni maneno ya wahenga. Ah! Tuyaache hayo ya Mhenga na Wahenga ambayo yametawala, lakini pia kuna hili la ujio wa timu ya Everton ambalo ilitikisa mji.

Kiukweli mchezaji pekee niliyemfahamu alikuwa ni raia wa Congo DRC, Yannick Bolasie, na huyu ni kwa ukaribu tu wa Congo na hapa kwetu. Lakini Wayne Rooney alipoamua kurudi nyumbani ndio sasa zikaamka shangwe na hamasa kila kona.

Haya Rooney huyo kaja na kaondoka, katuachia nini vijana au ndo katuachia kuvamia uwanja tu na kuondoka au tumejifunza aina ya uchezaji wake. Hivi ulikosa namna ingine ya kutafuta umaarufu hadi uamue kufanya ulivyo fanya, ni hatari sana ila askari wetu shupavu nanyie muache kuangalia mpira na sasa muwageukie mashabiki na kuangalia maana lile doa kwenu, mjisahihishe. Mimi naamini tumejifunza kitu, na kitaleta mabadiliko hasa kwa vijana wasakata kabumbu.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Mroki Mroki

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi