loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vijiji 2 kumezwa ujenzi bwawa la Farkwa

Hayo yalibainishwa juzi wakati wa kikao cha tathmini ya athari kwa mazingira na jamii ya mradi wa bwawa la Farkwa na mfumo wake wa kupeleka maji Manispaa ya Dodoma.

Kulingana na utafiti uliofanyika bwawa hilo litatoa maji kwa muda wa miaka 20. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Francis Isack vijiji hivyo ni Bubutole na Mombose alisema vijiji hivyo vitaondolewa kupisha bwawa na wananchi wataamua pa kwenda.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya aliwaambia wadau kuwa hakuna tamko maalumu hivi sasa kuhusu vijiji hivyo.

Alisema fidia italipwa na Wizara ya Maji na halmashauri itasimamia na sasa kinachofanyika ni kujua nani yuko wapi na ana nini. Mtaalamu mshauri wa mradi huo, kutoka Kampuni ya Tres, Bashiru Hassan alisema bwawa litafungwa chini ya makutano ya mto Bubu na Mkinki.

Alisema maji yatafurika na kumeza sehemu kubwa ya vijiji vya Mombose na Bubutole na mabomba yatatandazwa kulepeka maji Manispaa ya Dodoma umbali wa kilomita 130 na vijiji kando ya bomba vitapata maji.

Alisema kulingana na maoni ya wadau waliuona mradi ni mzuri na utaweza kumaliza tatizo la maji katika Mji wa Dodoma na vijiji ambavyo mradi huo utapita.

Pia mradi huo utakuza shughuli za kijamii na kuimarisha maendeleo katika eneo hilo na angalizo kubwa ni juu ya ulipaji wa fidia kwa muda.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewataka wasanifu wa mradi huo kubadilisha usanifu ili vijiji vilivyo kilomita 12.5 utakapopita mradi huo vipate maji.

Pia alisema Serikali itasanifu upya mradi wa umwagiliaji ili maji yaweze kutumika kwa umwagiliaji kwa upande wa Vijiji vya Wilaya ya Bahi ambavyo vipo chini ya eneo la bwawa ambapo mto Bubu ulikuwa unaelekea.

Alisema tayari suala la kulipa fidia watu watakaopitiwa na mradi huo limeanza kushughulikiwa. Na kutaka maji hayo pia yasambazwe katika wilaya ya Bahi, Chamwino, na Chemba.

Pia alitaka kuangaliwa namna ya kutibu maji ili kuondoa wadudu, fangasi na bakteria badala ya kufunga mitambo mikubwa ya kusafishia maji na badala yake maji yanayokwenda Bahi, Chemba, Dodoma na Chamwino yatibiwe huko ili maji ambayo hayajatibiwa yatumike kwa umwagiliaji.

Alisema sasa Serikali imeanza kufanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) ili waweze kupata fedha za kuanza mradi wa ujenzi pindi usanifu utakapokamilika. Aliagiza kuoteshwa kwa samaki katika bwawa hilo ili wavuvi wafaidike zaidi na bwawa hilo.

WASHEREHESHAJI katika matukio mbalimbali zikiwamo sherehe za harusi, ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi