loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Viongozi CCM acheni kuwaza urais'

Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati alipozungumza na wajumbe wa kamati za siasa za majimbo Mkoa wa Kaskazini Unguja, eneo la Mahonda.

Alisema hakuna sababu ya kuanza harakati hizo wakati huu kwani rais atapatikana tu lakini kazi kubwa inayokikabili chama kwa sasa ni kutafuta wapiga kura wapya watakaokipa ushindi chama hicho.

Vuai alisisitiza suala la viongozi wa chama kuitisha vikao kuanzia shina hadi tawi ambavyo ndiyo vitakavyozipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na wanachama.

“Hili limenisikitisha sana, wananchi wamekuja ofisini kwangu kunilalamikia kwamba wapo wabunge na wawakilishi wameshindwa hata kutoa shukrani tangu walipochaguliwa sasa zaidi ya miaka mitatu, haipendezi hata kidogo hizo ndizo kasoro zinazotukosesha ushindi,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu wa Idara ya Utikadi na Uenezi ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwataka viongozi kutekeleza ahadi zao wanazozitoa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Alisema miongoni mwa malalamiko makubwa ya wananchi katika majimbo ya uchaguzi ni viongozi kushindwa kutekeleza ahadi kwa wapiga kura.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Khamis Juma alisema ahadi nyingi za Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi mkoani humo zimefanyika na kero nyingi zimepatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la maji safi na salama.

Kwa mfano alisema wananchi wa Matemwe kilio cha ukosefu wa maji safi na salama sasa kimepata ufumbuzi ambapo huduma hiyo inapatikana.

MABALOZI wawili wa nchi za Marekani na Vietnam waliowasilisha hati ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi