loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viongozi wa dini waaswa kuisaidia Serikali

Ombi hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya jana.

Choya alikuwa akifunga mkutano wa kuliombea Taifa ulioandaliwa na asasi ya The new Life in Christ na kufanyika kwenye uwanja wa Kwaraa mjini hapa.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema Serikali inatambua umuhimu na mchango wa makanisa katika kuleta amani na upendo miongoni mwa wananchi na kwamba viongozi wa dini ni viyoyozi vinavyosaidia kuwapepea baadhi ya wanasiasa wenye uchungu usio wa kweli na nchi yao.

Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo viongozi wa dini wanapaswa kuisaidia Serikali katika kukabiliana nazo kuwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa vijana, wazee na waumini pamoja na vurugu katika baadhi ya makanisa.

Aidha, alitaja changamoto nyingine kuwa ni rushwa aliyosema kuwa ni janga linaloendelea kuitafuna nchi.

Akawaomba viongozi wa dini kuwafichua wala rushwa wote kwani ni waumini kwenye makanisa yao na kuwakemea, kuwaonya na kuwaombea ili wasiendelee na tabia hiyo.

Kiongozi huyo alisema Mkoa wa Manyara umekuwa ukikabiliwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo imesababisha hata wanafamilia kufarakana.

Aliwataka kumaliza migogoro hiyo kwa mazungumzo badala ya kuipeleka kwenye vyombo vya sheria ili kuendeleza amani ndani ya familia na Mkoa wa Manyara kwa ujumla.

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi