loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Vituo vikubwa vya matibabu vya NHIF mbioni kukamilika

Hayo yalibainika jana wakati wa matembezi ya waandishi wa habari katika miradi miwili mikubwa, inayojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Dodoma.

Miradi hiyo miwili ni ya kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Kituo cha mfano cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Miradi yote miwili hiyo inajengwa kwa thamani ya Sh bilioni 48, ambapo kituo cha mfano kilichopo hospitali ya rufaa kinajengwa kwa Sh bilioni sita na sasa kipo tayari, mkandarasi anamalizia vitu vidogo vilivyobaki.

Mhandisi wa NHIF, Simon Seleman amesema kwamba kituo cha kisasa cha UDOM ambacho kikimalizika kitagharimu Sh bilioni 43, kwa sasa kipo katika hatua ya asilimia 95 na kwamba kazi zilizobaki zinasubiri kuwasili kwa vifaa tiba ili kukamilisha ujenzi.

Vifaa tiba vinavyokusudiwa vina thamani ya Sh bilioni 23. Mhandisi huyo alisema miradi yote hiyo yenye awamu mbili itakapokuwa kamili ni msaada mkubwa kwa wanachama na wananchi.

Awamu ya pili ya kituo cha UDOM, itakuwa ni ujenzi wa hospitali ambayo itakuwa na vitanda 300 na itakayotumiwa na wanafunzi wa Kitivo cha Tiba cha UDOM.

Aidha, katika kituo kilichopo hospitali ya rufaa katika awamu ya pili kutajengwa mochwari ya kisasa yenye uwezo wa kuhifadhi miili 30, kichomea taka na eneo la kufulia nguo za hospitali.

Pia, wagonjwa kati ya 700 hadi 800 wanatarajiwa kuhudumiwa kwa siku na kituo cha uchunguzi wa magonjwa cha Dodoma kitakapoanza kazi mapema mwakani.

Kwa mujibu wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Dodoma (UDOM) anayeshughulikia mipango, fedha na utawala, Profesa Shaban Mlacha, kituo hicho ambacho kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya figo, kina maabara ya kisasa na vifaa vya kisasa huku kukiwa na vyumba 40 vya madaktari.

Aidha, Profesa Mlacha akizungumza alisema kwamba kuwapo kwa kituo hicho na hospitali itakayojengwa itachangia si tu katika kufanya utafiti wa magonjwa na kutibia, lakini pia itatoa nafasi kwa wanafunzi wa kitivo cha tiba UDOM na walimu wao kufanya mazoezi yanayostahili na kuonesha ubingwa wao.

Taarifa ya mjenzi, Habibu Nuru wa Hab Consult Limited anayejenga kituo hicho, ilisema hadi sasa wamefikia asilimia 95 na ni moja ya majengo ambayo taifa inaweza kujivunia.

Fedha hizo zote zinatoka katika Mfuko wa Bima kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanachama wake wanatibiwa vyema na wananchi wapata huduma pia.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya akizungumzia kituo cha mfano, alisema matarajio yake kuwa kitaongeza idadi ya wanachama wa NHIF wanaohudumiwa hospitalini hapo kutoka idadi ya wagonjwa hamsini wanaotibiwa sasa.

Alisema ujenzi wa kituo hicho, utaondoa changamoto zilizopo kama za msongamano za watu waliokuwa wakitumia kadi za bima ya afya. Watu hao walikuwa na chumba kimoja tu katika hospitali hiyo ya rufaa.

Pamoja na ujenzi wa kituo hicho, bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto za madaktari bingwa, ambao pia wanatakiwa kufanya kazi katika kituo hicho kipya.

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi