loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Vyandarua vya hati punguzo vyasitishwa

Mpango huo ulioanza mwaka 2004 , umesitishwa mwezi uliopita baada ya serikali kwa kushirikiana na wadau wake, ikiwemo shirika lililokuwa likiusimamia, kugundua kuwepo udanganyifu mkubwa.

Mpango huo ulianzishwa kuhakikisha wajawazito na watoto wachanga, wanaendelea kupata vyandarua vyenye viuatilifu kwa gharama nafuu, kuwakinga na maambukizi ya malaria.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe amesema waligundua udanganyifu mkubwa wa utekelezaji mpango hasa wa kielektroniki, uliosababisha watu wasio walengwa kupata vyandarua na kuviuza.

“Udanganyifu huo umefanywa na baadhi ya watumishi wa serikali na maduka binafsi wasio waaminifu kwa kutoa hati hewa kwenye mfumo wa kutoa chandarua kwa watu ambao siyo walengo wa mpango kisha kujipatia fedha isivyo halali,” alisema Naibu Waziri.

“Serikali ya Uingereza ambao ndio wafadhili wa mpango kwa sasa, wamesitisha ufadhili huo. Jambo hili ni la kusikitisha na halikubaliki,” alisema.

Alisisitiza, “Serikali inachukua hatua za dharura na madhubuti, kukabiliana nalo kwa kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote watakaothibitika kuhusika na wizi huu.”

Dk Kebwe alisema jambo hili ni la kusikitisha na halikubaliki, hivyo serikali inachukua hatua za dharura na madhubuti, kukabiliana nalo kwa kufanya uchunguzi wa kina kuchukua hatua za kinidhamu kwa wote watakaothibitika kuhusika na wizi huo.

Shirika la Mennonite Economic Development Associates (Meda), ndilo lilikuwa likisimamia utekelezaji wa mpango huo.

Pengo lazibwa

Hata hivyo, Naibu Waziri alisema wanafanya majadiliano na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo (DFID), kuandaa utaratibu mpya vyandarua.

Alisema wameonesha nia ya kushirikiana na serikali katika utaratibu huo mpya, utakaotayarishwa, lengo likiwa ni kupambana na ugonjwa wa malaria. Aliomba umma uondoe wasiwasi, akisema vyandarua vitaendelea kutolewa kama ilivyopangwa.

Kulingana na maelezo ya Dk Kebwe, wamepanga Aprili mwakani mpango mpya utakapoanza, kuwe na utaratibu mpya wa ugawaji wa vyandarua hivyo vyenye viuatilifu vya muda mrefu usioruhusu mianya ya udanganyifu.

Rasimu hiyo ya utaratibu wa usambazaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu, itaainisha na kuhakikisha mafanikio yanakuwa endelevu hususani kusambaza vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito na watoto, mifumo ya bima ya afya, kupitia wanafunzi shuleni na sekta binafsi.

Serikali imesisitiza maandalizi ya mpango mpya kuziba pengo, litakalotokana na kusitishwa kwa huo uliokuwa ukifadhiliwa na Meda. Imesema katika mpango ujao, jamii yote itanufaika. Mpango huo unaokuja, utaendelea kunufaisha wajawazito.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, amewataka ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi