loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waandishi wengi hawana bima

Kauli hiyo ilitolewa leo na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Maryam Salum Msabaha (Chadema).

Nkamia alisema; “ni kweli waandishi wa habari wengi, hawana bima kwa sasa. Suala hili la bima ni suala linalohusu maamuzi ya mtu binafsi, yaani mwandishi wa habari mwenyewe.

“Nia ya Serikali katika Muswada wa Sheria Mpya ya Kusimamia Vyombo vya Habari, unaotarajiwa kuletwa mbele ya Bunge lako tukufu ni kuhakikisha kuwa inaweka sharti kwa waajiri wote kuwawekea au kuwakatia bima watumishi wao.

“Aidha, waandishi wa habari wa kujitegemea nao pia watalazimika kujikatia bima ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi,” alisema Naibu Waziri.

Nkamia alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango, unaotolewa na waandishi wa habari nchini katika kutoa habari, kuelimisha na kuburudisha jamii. Alisema mchango huo umesaidia katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi