loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waaswa kudumisha moyo wa muungano

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan ametoa rai hiyo juzi wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya kuwaaga wastaafu 12 wa kada ya maofisa katika ofisi hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.

“Natambua kwamba ninyi nyote mliostaafu na mtakaostaafu ni mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii kuhusu majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yanayohusu kuudumisha Muungano wetu pamoja na kuhifadhi mazingira,” alisema.

Aidha, aliwaasa wastaafu hao kushirikiana na Asasi na Taasisi mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao ili kupitisha mawazo ambayo yatasaidia kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa wale wanaoendelea na utumishi wa umma Waziri Samia aliwataka waige mfano kwa watumishi waliostaafu na kuendelea kujenga tabia ya uadilifu, uaminifu na uchapakazi.

Wastaafu hao walipatiwa zawadi ya jiko la gesi kila mmoja jambo ambalo Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Angelina Madete alipokuwa akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi alisema ofisi iliandaa zawadi hiyo ili wastaafu hao wakawe mabalozi wazuri wa kuhimiza matumizi ya jiko la gesi na hivyo kusaidia katika uhifadhi wa mazingira.

RAIS John Magufuli amewataka wasaidizi wake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi