loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waaswa kuepuka wanasiasa wenye uchu wa madaraka

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Manispaa ya Moshi, Priscus Tarimo alisema hayo hivi karibuni alipokuwa anazungumza na wanachama wa Vicoba Kimoka, Kata ya Bomambuzi kilichotoa msaada wa chakula kwa wazee wa kata hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Tarimo, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Manispaa ya Moshi, Abdallah Thabit, alisema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, baadhi ya wanasiasa hutoa kauli za vitisho, hivyo hawastahili kuungwa mkono.

Kuhusu masuala ya kiuchumi, Tarimo alitaka vikundi vya vijana na wanawake katika manispaa hiyo kuandaa andiko la mradi na kuwasilisha katika ofisi hizo kwa ajili ya kuomba mikopo ili kujiimarisha kiuchumi badala ya kutegemea misaada zaidi.

Alisema kila halmashauri nchini inalazimika kwa mujibu wa sheria kutenga asilimia 10 kwa vijana na wanawake kwa ajili ya utoaji mikopo hivyo wao wanastahili kufuata taratibu ili wanufaike na mikopo hiyo.

Mapema katika taarifa yake kwa katibu huyo, Katibu wa Kimoka, Khadija Msengi alisema kikundi hicho kinatarajia kuanzisha mradi wa kiuchumi wa kukodisha hema utakaogharimu zaidi ya Sh milioni 2 ambao itakuwa ni sehemu ya kitega uchumi cha kikundi.

Aidha, Katibu huyo alisema kikundi chake cha wanachama 43 pamoja na kutoa msaada kwa wazee 25 waliopata mchele, sabuni na sukari, lakini pia kinatarajia kutoa elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha wanawake kukopo na kuanzisha miradi endelevu. Pamoja na miradi ya kiuchumi, lakini pia tayari Kimoka imesaidia wanachama wake katika matatizo ya aina mbalimbali ikiwamo maradhi, misiba na mafuriko na kwamba lengo ni kuhakikisha ni kubadili maisha ya wanajamii wake.

Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi ...

foto
Mwandishi: Nakajumo James, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi