loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wabunge, wizara wadaiwa shilingi milioni 816 na TBA

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Maua Daftari (CCM). Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inasema nini juu ya ubovu wa nyumba nyingi za TBA.

Pia, alihoji kwa nini jukumu hilo la TBA kwa Dodoma lisibinafsishwe, akapewa mtu mwingine na kuliendesha na kukarabati nyumba zake ili wapangaji wake waishi kwa usalama.

Akijibu swali hilo, Lwenge alisema upungufu wa fedha za matengenezo ya nyumba unachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wapangaji, wakiwemo wabunge, wizara na taasisi za Serikali kutolipa kodi ya pango kwa wakati.

“Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Septemba, mwaka huu, TBA Mkoa wa Dodoma inawadai wateja wake malimbikizo ya kodi yanayofikia Sh 816,827,577. Hivyo nichukue nafasi hii kuwaomba wadaiwa wote walipe ili TBA iweze kupata fedha za kukarabati nyumba zake,” alisema.

Kuhusu kubinafsishwa kwa nyumba hizo, alisema mapendekezo ya kubinafsishwa uendeshaji na ukarabati wa nyumba za TBA za Dodoma kwa mtu au kampuni binafsi, si suluhisho la kufanya matengenezo ya nyumba hizo kwa wakati, kwa kuwa lengo la kuanzisha TBA limezingatia Sheria Namba 30 ya mwaka 1997.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewashauri watendaji ...

foto
Mwandishi: Oscar Mbuza

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi