loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wachezaji 251 wajitokeza majaribio Ruvu Shooting

Wachezaji 251 wajitokeza majaribio Ruvu Shooting

Akizungumza na wachezaji hao kwenye Uwanja wa Ruvu, Kocha Mkuu, Tom Olaba alisema lengo la kutangaza nafasi hiyo ya kuwaita wachezaji ni kuwapatia fursa chipukizi wenye uwezo wa kusakata soka ili watoe mchango wao kwenye kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu msimu ujao.

Olaba alisema wamewaita wachezaji hao kufanya majaribio ili watakaofuzu majaribio hayo wapate nafasi ya kuitumikia Ruvu Shooting, hivyo wanapaswa kuonesha uwezo na watakaofaulu watapata nafasi bila ya upendeleo.

“Mazoezi haya yataendelea kwa wiki mbili ambayo yatakuwa yanachezwa kwa mtindo wa bonanza ikiwa na lengo la kuwapatia nafasi nzuri zaidi wachezaji kuonesha uwezo wao wa kucheza soka na hatimaye wapatikane wachezaji wenye vipaji,” alisema Olaba, raia wa Kenya.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Ruvu kilichopo timu hiyo, Luteni Kanali Charles Mbuge alisema uongozi huo unaendelea kuwataka vijana zaidi wajitokeze kwani lengo ni kuhakikisha wanapata wachezaji wenye uwezo watakaosajiliwa kwa ajili ya Ligi Kuu na wale wenye chini ya umri wa miaka 20.

“Lengo kubwa ni kuhakikisha tunapata wachezaji ambao wataisaidia timu ili iweze kufanya vyema kwenye ligi ijayo pamoja na kuwaandaa vijana wengine watakaoitumikia timu miaka ya baadaye kwenyeligi zijazo,” alisema Luteni Kanali Mbuge.

Alitoa shukrani kwa jopo la makocha Olaba na msaidizi wake, Seleman Mtungwe waliojipanga vizuri katika kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kama lilivyopangwa na hatimaye kupatikana kwa wachezaji bora zaidi watakaoongezea ushindani katika kikosi hicho kwenye kinyang’anyiro kijacho.

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi