loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachezaji waomba mshikamano Simba

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Simba kufanya vibaya kwenye mechi yao dhidi ya Ruvu JKT kwa kutandikwa mabao 3-2, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Chollo alisema kikosi chao kwa sasa kiko kwenye wakati mgumu, ni muhimu wanachama wa Simba wakashikamana na kuwaunga mkono kipindi hiki kigumu kwao, ili kufanya vizuri katika michezo inayokuja.

Alisema ni haki ya wanachama kulalamika kwamba timu haifanyi vizuri kwa sababu wana uchungu nayo, lakini akawakumbusha kuwa sio kwamba wanapenda kufanya vibaya, hata wao pia wanaumia isipokuwa matokeo siku zote hubadilika.

“Ni haki ya wanachama kuwalaumu wachezaji, viongozi lakini twende mbele na kufikiria kuwa katika mchezo siku zote usitarajie kushinda, kuna kufungwa na kutoka sare pia, ndivyo ulivyo, tuko katika wakati mgumu,” alisema.

Chollo alihimiza wachezaji wenzake kujitambua katika kipindi hiki kigumu kwa kujitahidi kufanya vizuri katika mechi zijazo ili kubaki katika nafasi nzuri.

Kuhusu kutokuelewana kati yao na Kocha Zdravko Logarusic alisema anavyofundisha kwa mtu ambaye umelelewa katika utamaduni tofauti, anapozungumza jambo wakati mwingine unaweza kuchukulia kama tusi lakini kumbe ndivyo kocha alivyozoea.

Mchezaji huyo hakucheza tangu kuanza kwa mzunguko wa pili kutokana na kuwa majeruhi, lakini jana alisema kwamba yupo fiti na endapo atapangwa kwenye kikosi kitakachocheza na Ruvu Shooting Jumapili, atakuwa tayari kutoa mchango wake.

Naye Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi ili kuanzia mechi inayokuja dhidi ya Ruvu Shooting iweze kufanya vizuri na kuhakikisha wanabaki katika kiwango kizuri.

Wakati huo huo, Kamwaga aliwahimiza wanachama wa Simba kujitokeza Jumamosi asubuhi makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo wakiwa na majembe, mashoka na vifaa vingine kwa ajili ya kwenda kutengeneza uwanja wao ulioko Bunju.

Alisema baada ya wanachama kufyeka, watapeleka greda kuuweka uwanja huo sawa na ndani ya siku 100 watakuwa wamemaliza kuweka nyasi bandia ili kuwawezesha wachezaji kuanza kuutumia kwa mazoezi.

VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania, Azam FC ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi