loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wadau wa maendeleo tumieni taarifa za sensa

Pengine tunaweza kusema pia kwamba vita iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mara baada ya kupata uhuru Desemba 9, 1961 imeanza kuonesha matunda yake.

Vita hiyo ni dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini. Baadhi ya viashiria ambavyo taarifa hiyo imeonesha kwamba zimeboreshwa ni pamoja na umri wa kuishi ambao umepanda kutoka miaka 51 mwaka 2002 hadi kufikia miaka 61.

Wakati tulipopata uhuru umri wa kuishi wa Mtanzania ulikuwa miaka 37.5. Sambamba ni ongezeko la umri wa kuishi, makazi ya Watanzania yameboreka zaidi kwa maana ya vifaa thabiti vilivyotumika katika ujenzi.

Hivi sasa asilimia 62 ya nyumba za kuishi za Watanzania zimeezekwa kwa bati tofauti na mwaka 2002 ambapo ni asilimia 46 tu za nyumba za Watanzania ziliezekwa kwa bati. Kwa upande wa afya, vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka watoto 115 kati ya kila watoto hai 1,000 waliozaliwa mwaka 1988, hadi vifo 45 kwa kila watoto hai 1,000 waliozaliwa mwaka 2012.

Pia vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 231 mwaka 1998 hadi 68 ambapo mwaka 2013 vimefikia vifo 54 kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa hai.

Taarifa hiyo pia imeonesha ongezeka katika umiliki wa simu za kiganjani sasa umefikia asilimia 64 mwaka 2012 toka asilimia 10 mwaka 2005 huku umasikini nao ukiwa umepungua hadi kufikia asilimia 28.2.

Kipato pia kimepanda kutoka dola za Marekani 321 mwaka 2002 hadi kufikia dola 717. Kwa vyovyote vile, pamoja na ukweli kwamba bado tuna safari ndefu ya kufikia kwenye maendeleo bora zaidi kuliko tuliyonayo hivi sasa, ni ukweli pia kwamba tumepiga hatua ambayo sisi wenyewe na wenzetu wengine wanaweza kuona kwamba tunasonga mbele na siyo kama tulivyokuwa hapo awali. Kwa hili tuna haki ya kujipongeza.

Katika hili pia tunapenda kuungana na Rais Kikwete kuwasihi wananchi, wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuzitumia takwimu hizo katika shughuli na mapango yao mbalimbali badala ya kutumia taarifa za kubuni.

Suala la upotoshwaji lisipewe nafasi tena kwani kwa kufanya hivyo hatulisaidi taifa wala taasisi ambayo itatumia taarifa ambazo siyo rasmi.

Sambamba na hao, pia wizara zetu, taasisi za Serikali, Serikali za Mitaa Serikali Kuu zitumie ipasavyo taarifa hizo katika mikakati na mipango yake mbalimbali ya kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa letu.

Tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya matumizi sahihi ya taarifa hiyo kama inavyotarajiwa.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi