loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara wa Mchikichini poleni

Soko hilo lina wafanyabiashara zaidi ya 2,700 waliosajiliwa na hivyo kuwaacha katika hali tata ya kutokuwa na ajira ya kuweza kujikimu maisha yao ya kila siku kama ilivyokuwa kabla ya kutokea kwa janga hilo.

Tunapenda kuwapa pole wafanyabiashara hao kwa tukio hilo ambalo kwa kiasi kikubwa litawafanya wachukue muda mrefu kuweza kurudi katika hali yao ya kawaida katika harakati za kujitafutia kipato halali cha kujikimu wao na familia zao.

Tunampongeza Meya wa Ilala, Jerry Slaa kwa kitendo cha kuunga mkono wafanyabiashara hao kuendelea kutumia soko hilo hususani kwa wakati huu mgumu wa kuharibiwa kwa moto bidhaa zao.

Ni jambo la kutia moyo pia tamko la Mstahiki Meya kwamba Serikali itaendelea kuwasaidia wafanyabiashara hao katika kipindi hiki kigumu.

Lakini pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wafanyabiashara wa soko hilo, masoko mengine na hata jamii yote kwa ujumla wake kujenga utamaduni wa kujikatia bima dhidi ya majanga kama hayo ya moto.

Tumeambiwa kwamba wafanyabiashara katika soko hilo lililoteketea, karibu wote hawana bima yoyote dhidi ya ajali ya moto. Hili ni jambo la kusikitisha lakini pia liweze kutufumbua macho na kulichukulia tukio hilo kama changamoto kwa wafanyabiashara wote kuzingatia umuhimu wa kukata bima dhidi ya majanga mbalimbali.

Pamoja na ukweli kwamba uchunguzi bado unafanywa juu ya nini hasa kimesababisha moto huo, ni ukweli pia kwamba wafanyabiashara husika hawana budi kuwa makini wanapomaliza kazi zao za siku na kurejea makwao kwa kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya umeme na vile ambavyo ni hatari kusababisha kuzuka kwa moto vimechekiwa na kuzimwa inavyotakiwa kabla ya kuondoka.

Tukijenga utamaduni wa aina hii na kukumbusha miongoni mwa wafanyabiashara waliopo jirani kuhusu kuacha ofisi katika hali ya usalama dhidi ya janga la moto na mengine kutasaidia kupunguza majanga kama hayo na kufanya maeneo ya kufanyia kazi na biashara kuwa salama kwa kiasi kikubwa.

Haitakuwa jambo baya pia kuhakikisha kwamba walinzi nao wa maeneo husika kujenga pia utamaduni wa kuwakumbusha wafanyabiashara kuzingatia masuala ya msingi ya kiusalama ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuzuka kwa moto na hata wizi katika maeneo ya kazi.

Tunaamini kwamba kama pande zote zinazohusika katika maeneo hayo ya biashara wakizingatia masuala ya kiusalama, majanga kama hayo yatadhibitiwa inavyostahili na hivyo sote kubaki salama kuendelea na shughuli zetu za kutuingizia kipato.

Mshikamano katika hili ni muhimu kuweza kulifanikisha suala la udhibiti wa majanga kama ya moto.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi