loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafuasi 17 wa Chadema kortini kwa kutotii amri

Washitakiwa hao ni Katibu wa Chadema mkoa wa Katavi, Almasi Ntije (34), Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Abrahamu Mapunda (61) na Katibu wa Chadema wa Jimbo la Mpanda Mjini, Cretus Nkumba.

Wengine ni Hamisi Korongo (40), Lameck Constantino (37), Mlokozi Bagasheki (30) , Shaban Ibrahim (26), Kennedy (20), Francis Misngalo (29) , Seleman Hamis (25) , Kasena Maulid (29), Mailwa James (25), Emil Kamolo (50), Seif Ibrahim akiwemo mwanamke pekee Mariam Omary (45) ambao wanadaiwa kuwa wafuasi wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alidai washtakiwa hao walikamatwa jana saa nne asubuhi wakiwa katika eneo la zahanati ya Kasimba, Mtaa wa Majengo A mjini hapa.

Alieleza kuwa walikuwa wanaandamana kuelekea katika viwanja vya Hoteli ya Mpanda ambako ulitarajiwa kufanyika mkutano wa hadhara.

Katika kamata kamata hiyo kwa mujibu wa Kidavashari, wafuasi wengine ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walifanikiwa kutoroka.

Awali viongozi wa chama hicho waliandika barua Septemba 22, mwaka huu kwa jeshi la polisi wilaya ya Mpanda wakiomba kibali ili waweze kufanya maandamano Septemba 25 pamoja na mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Hoteli ya Mpanda.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda liliwajibu barua hiyo Septemba 24 ikikitaka chama hicho kisifanye maandamano wala mkutano wa hadhara.

Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda, Idd Faraja alieleza kuwa chama hicho kiliamua kufanya maandamano hayo baada ya Jeshi la Polisi kuchelewa kuwapatia barua ya kuwazuia kufanya maandamano na mkutano wa hadhara.

Alisema kitendo cha polisi kuchelewa kujibu barua yao ya kuomba kibali walivyoona imekuwa kimya walijua kuwa wamekubaliwa.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mpanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi